.

MZEE MANGULA ANOGESHA SEMINA YA VIJANA WA UVCCM TAWI LA VYUO NA VYUO VYA ELIMU YA JUU ST JOSEPH LEO

Feb 18, 2018

 Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula akizungumza katika Kongamano la Miaka 41  ya CCM, kwa Vijana wa CCM wa  Vyuo na Vyuo Vikuu Tawi la Chuo cha St. Joseph, Seneti ya Dar es Salaam, iliyofanyika leo Feb 18, 2018 katika ukumbi uliopo Mbezi, Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku na wengine kutoka kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Idara ya Vyuo na vyuo Vikuu UVCCM Daniel Zenda, Katibu wa CCM Wilaya ya Ubungo Salum Kalii na Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Chuo cha St. Joseph Ikram Soragha. Akizungumza amesema yeye na viongozi wengine wenye umri mkubwa wanafarijika sana wanapoona vijana 'wanatroti' kupokea kijiti cha uongozi kutoka kwao, kwa kuwa wakikabidhiwa vijiti hivyo bila kuwa tayari hawatakuwa na manufaa kwa Taifa
 Baadhi ya vijana wakiwa kwenye semina hiyo
 Vijana wakihamasisha wenzao wakati Makamu Mwenyekiti wa CCM -Bara Philip Mangula hajafika ukumbini
 Vijana wakionekana kuwa na hamasa wakati wakimsubiri Mzee Mangula kwasili ukumbini
 Kijana akihamasisha wenzake kwa wimbo wakati wakimsubiri Mzee Mangula kuingia ukumbini
 Katibu wa CCM Willaya ya Ubungo Salum Kalii akishauriana jambo na Kaimu Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM, Taifa Daniel Zenda wakati wa semina hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Chuo cha St. Joseph Ikram Soragha.
 Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye semina hiyo
 Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Chuo cha St. Joseph Ikram Soragha akifungua kikao cha semina hiyo
 Kaimu Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu UVCCM Taifa Daniel Zenda akifanya utambulisho wa wenyeji
 Kattibu wa CCM Wilaya ya Ubungo Salum Kalii akitoa neno la Utangulizi na kumkaribisha Mzee Mangula kuzungumza na washiriki wa semina hiyo 
 Mzee Mangula akizungumza na washiriki wa semina hiyo ya miaka 41 ya CCM. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku akitoa mada kuhusu Maana ya Itikadi, akasema "Huwezi kujua Itikadi ya Chama chako kama hujui historia ya nchi ilikoto". 
 "Ni lazima msome vitambu mbalimbali kuhusu historia ya nchi, mfano wa vitabu hivyo ni hiki cha Azimio la Arusha", alisema Butiku huku akionyesha kitabu hicho
 Mzee Mangula akimpongeza Mzee Butiku kwa kutoa mada iliyoshiba, kwenye semina hiyo
 Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa UVCCM Tawi la Chuo cha St. Joseph Ikram Soragha, wakati kijana huyo akimshauri jambo kwenye semina hiyo. 
 Mpigapicha mahiri wa Televisheni ya Taifa (TBC1) George Kasembe akiwa kazini wakati wa semina hiyo
 Mzee Samuel Kaseri akitoa mada kuhusu Itikadi kwenye semina hiyo
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula akifafanua mambo mbalimbali mwishoni mwa Kongamano la Miaka 41  ya CCM, kwa Vijana wa CCM wa  Vyuo na Vyuo Vikuu Tawi la Chuo cha St. Joseph, Seneti ya Dar es Salaam, iliyofanyika leo Feb 18, 2018 katika ukumbi uliopo Mbezi, Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª