.

TARATIBU ZA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA KWA WANACHAMA WA MIFUKO YA JAMII NCHINI

Feb 2, 2018

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inawajulisha wanachama wote wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini watakaosajiliwa kupata Vitambulisho vya Taifa kuzingatia yafuatayo:-

 Watakaosajiliwa ni watu wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, Raia wa Tanzania na wageni wanaoishi kihalali nchini na awe mwanachama wa mfumo wa Hifadhi ya Jamii.

 Fomu za kujisaji zinapatikana kwa mwajiri wako, Ofisi ya Serikali ya Mtaa unakoishi au Ofisi ya NIDA na hakikisha umejaza fomu hiyo vipengele vyote kwa kalamu nyeusi na kuweka viambatisho muhimu vitakavyokutambulisha Umri, Makazi na Uraia. Vielelezo hivyo ni Cheti cha Kuzaliwa, Pasi ya kusafiria (Passport), vyeti vya shule ( Msingi, Sekondari), Leseni ya Udereva, Kadi ya Bima ya Afya, Kadi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi na Kitambulisho cha Kupigia Kura na kitambulisho cha kazi.

Kuwa na Viambatisho vingi zaidi ni kutambulika kwa haraka zaidi. (Viambatisho vyote ulivyonavyo vitoe nakala (photocopy) na kuambatisha na fomu yako ya maombi kwa ajili ya hatua ya kupigwa picha, kuchukuliwa alama za vidole)
 Kwa wageni wawe na Passport ya nchi alikotoka, kibali cha kuishi nchini na kibali cha kufanya kazi vinavyotolewa na Serikali.

 Hakikisha fomu yako kipengele namba 59 umesaini wewe, No. 60 - Kimejazwa na Mwenyekiti au mtendaji wa Mtaa unaoishi na Kipengele Na.70 – kimejazwa na Mwajiri.
 Baada ya kukamilisha hatua za awali za Usajili kutakuwa na hatua ya Uhakiki wa Taarifa na mapingamizi.

Uchukuaji alama za Vidole, Picha na Saini ya Kielektroniki utafanyika kuanzia tarehe 05 /02 hadi 28/02/2018 kwenye vituo vifuatavyo :-

 Ilala – Ofisi za PSPF, Jengo la Golden Jubilee, Mtaa wa Ohio
 Kinondoni – Ofisi za LAPF Jengo la Millennium Tower, Kijitonyama
 Temeke – Ofisi za PPF, Tazara
 Ubungo – Ofisi za GEPF Ubungo Plaza
 Kigamboni – Ofisi za NSSF, Darajani

Unapofika kwenye kituo unashauriwa kwa ubora wa picha usivae nguo nyeupe, bluu, pinki au nguo yoyote inayoshabihiana na nyeupe, kupata hina kwenye vidole, kuvaa kofia au T-shirts zenye maandishi/ michezo au kuvaa kofia.

Vitambulisho vya Taifa kwa Malendeleo ya Taifa

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช