.

MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE YAKABIDHI GARI KWA KITUO CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI, LEO

Feb 2, 2018

 Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kushoto) akimkabidhi funguo ya gari, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania, Thobias Andengenye katika hafla iliyofanyika leo kwenye Kituo cha Zimamoto cha Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania, Thobias Andengenye akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela katika picha ya pamoja na maafisa wa kikosi hicho na menejimenti ya TAA 
 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani cha Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi. Irene Sikumbili (kushoto) akiagana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye leo baada ya kukabidhiwa gari litakalotumiwa na Kamanda wa kikosi cha Zimamoto cha Viwanja vya Ndege Tanzania. Wengine kulia ni Mkuu wa Idara ya Manunuzi na Ugavi Bw. Mtengela Hanga na (katikati) Mkuu wa Idara ya Udhibiti Viwango Bw. Paul Rwegasha
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (kulia) akiagana na makamanda wa kikosi cha zimamoto na Uokoaji baada ya kukabidhi gari leo

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª