.

BALOZI WA KUWAIT AZURU SHULE YA SEKONDARI YA OLD TANGA NA KUZINDUA SHUGHULI MBALIMBALI

Mar 22, 2018


Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem alifanya ziara   katika Shule ya Sekondari ya Old Tanga na kuzingua kituo cha kompyuta ikiwa ni mwendelezo wa mradi ulionzishwa na Ubalozi huo unaofahamika kwa jila la “KITUO CHA KOMPYUTA KATIKA KILA TAASISI YA ELIMU”. Hiki ni kituo cha pili kuzinduliwa na Ubalozi tangu mwezi Agosti mwaka 2017 ambapo kituo cha kwanza kilizunduliwa katika Taasisi ya Taaluma Chuo Kikuu Dar es Salaam.

Kituo cha Kompyuta katika Shule ya Old Tanga kimeunganishwa na huduma ya mtandao ili kuhamasisha wanafunzi juu ya matumizi ya teknolojia kwa kupitia kompyuta zinazopatikana ndani yake ili kufanikisha utekelezaji wa mipango ya elimu kwa njia za kieloktroniki

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª