Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania,
Mh. Jasem Al-Najem (wa kwanza kulia) akizindua kisima cha maji katika
shule Gezaulole. akiwa na mwalimu Mkuu Maryam Shaban (wa tatu kulia), na
Sheikh Kaporo ambaye ni msimamizi wa ujenzi wa kisima wa kwanza
kushoto
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania,
Mh. Jasem Al-Najem akihutubia baada ya uzinduzi wa kisima, kulia kwake
ni Diwani wa Sumangila Fransis Chichi na kushoto kwake ni Mwalimu Mkuu
Waryam Shabani.
Diwani wa Sumangila, Fransis Chichi akizungumza jmbo mara baad ya Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Mh. Jasem Al-Najem kuzindua kisima
Wanafunzi wakiwa wamebeba vifaa maalumu vya kuhifadhi maji vilivyotolewa msaada na Ubalozi wa Kuwait Nchini
Balozi wa Kuwait Nchini Tanznia,
Mh.Jasem Al-Najem akiwa amekaa na kuzungumza na wanafunzi wa darasa la
kwanza shule ya Gezaulole ambapo amewaahidi kuwapati mdftari na mikoba
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Mh.Jasem Al-Najem katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule hiyo
Balozi wa Kuwait Nchini Tanznia, Mh.Jasem Al-Najem ajumuika na wanafunzi darasani na kukagua madftri yao
Wanafunzi wakiimba wimbo wa Taifa kwa kumkaribisha mgeni rasmi Mh, Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania, Mh. Jasem Al-Najem.
Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe, Jasem
Al-Najem azindua kisima cha 61katika shule ya msingi ya Gezaulole,
Wilaya ya Kigamboni Dar es Salaam machi 7, 2018, Ikiwa ni mwendelezo wa
utekelezaji wa mradi wa ''Kisima cha Maji katika kila Shule'', Ulio
anzishwa na Ubalozi wa Kuwati mwishoni mwa mwaka 2016, Hafla ya uzinduzi
wa kisim hicho kilihudhuliw na Diwani wa Sumangila, Fransis Chichi,
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, Maziku Luhemeg, Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi (CCM), Gezaulole, Masiku Lupa, Mwalimu Mkuu Maryam Shabani
pamoja na walimu na wanafunzi wa shule hiyo,kilicho zindiuliwa na Balozi
wa Kuwait Nchini Tanzania Mh. Jasem
Al-Najem. Ambapo kitanufaisha shule ya Msingi ya Gezaulole
iliyoanzishwa mwaka 1962 yenye wanafunzi 868 na madarasa kumi na shule
jirani ya Sekondari ya Ibnu Rushyyenye wanafunzi 250 iliyo anzishwa
mwaka 2007.
Balozi
wa Kuwait Nchini Tanznia, Mh. Jasem Al-Najem katika hotuba yake baada
ya uzinduzi huo amesema kuwa Ubalozi wa nchini mwake umeanzisha mradi wa
"Kisima cha Maji" ilikuitikia wito na kuunga mkono sera ya Rais wa
Tanzania, Mh. Jonh Magufuli ya kutoa Elimu bure .
Balozi Mhe, Jasem
Al-Najem ameeleza kuwa kuwa atashirikiana na viongozi wa eneo hilo
katika kutatua changamoto zitakazo kabiliana na shule hiyo,
Aidha
aliahidi kuwapatia wanafunzi wa shule hiyo, madaftari , , mikoba na
vifaa vya kuhifadhia maji kwa kila darasa ili wanafunzi wasihangaike
kuchukua maji katika kisima mara kwa mara huku akiwataka wanafunzi hao
kujihimu katika masomo yao ili wawe mdaktari, wanahabari, walimu.
Diwani
Sumangila kwa upande wake Francis Chichi ameishukuru Kuwait kwa
kuwachimbia kisima cha maji katika shule hiyo huku akimuomba Balozi, Jasem Al-Najem
kusaidia Kata yake gari la kubebea wagonjwa ili kuwaondolea akina mama
wajawzito na watu wazima ambao hulazimika kutembea masafa marefu kufika
Hospitali na katika vituo vya Afya ambapo baadhi yao wakati mwingine
hulazimika kukodi Pikipiki ili kufika huko, jambo ambalo linahatarisha
uhai wao
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269