.

MAMA MWANAMWEMA SHEIN AHUTUBIA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI VIWANJA VYA MAKUNDUCHI MKOA WA KUSINI UNGUJA LEO

Mar 8, 2018

 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiangalia nguo ilioshonwa na Kikundi cha Siri Moyoni Unguja Ukuu, wakati akitembelea maonesho ya Wanawake wa Mkoa wa Kusini Unguja kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani
 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimapata maelezo ya utengenezaji wa majiko na mikungu kwa kutumia malighafi ya udongo, akitowa maelezo Kiongozi wa Kikundi cha Tusitegeani Muyuni C Unguja,Bi. Fete Khamis wakati akitembelea maonesho ya Bidhaa za Wanawake katika viwanja vya makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja.
 WASANII wa Kikundi cha Zanzibar Roots cha Makombora wakionesha mchezo wa unyanyasaji wa Wanawake wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yalioadhimishwa Kitaifa katika viwanja vya Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja
 WANANCHI wa Mkoa wa Kusini Unguja wamejitokeza katika zoezi la uchangiaji wa Damu wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake katika viwanja vya Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja
 AFISA wa Save The Children Zanzibar,  Bingambo Maulid, akitowa maelezo ya kupinga udhalilishaji kwa Wanawake na Watoto wakati wa maonesho ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunianbi yaliofanyika katika viwanja vya Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja
 WANAFUNZI wa Skuli ya Msingi Makunduchi Mkoa wa Kusini Unguja wakishangilia wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliofanyika katika viwanja vya Makunduchi
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwahutubia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa hafla ya maadhimisho Siku ya Wanawake Duniani,huadhimishwa kila mwaka ifikapo March 8, maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.(Picha na Othman Maulid)

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª