Mkulima wa kutoka Kikundi cha Gezaulole kilichopo Msoga, Shabani Mbogo akielezea changamoto za kilimo katika eneo hilo. |
Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Pwani,Kapilima George (wa pili kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la Kikundi cha Gezaulole katika Kata ya Msoga. |
Mkulima Ally Mhenga akichangia jambo kuhusu changamoto za kilimo zinazowakabili.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Gezaulole, Ali Hussein akiangalia mbegu ya Wema.
Mkulima akisubiri majibu ya maswali yake kuhusu mbegu
ya Wema.
Matifiti Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu (wa nne kushoto), akielekeza namna ya kupanda mbegu hiyo kwa wanakikundi cha Gezaulole.
Hapa akielekeza vipimo vya upandaji wa mbegu hiyo.
Zoezi la upandaji wa mbegu hiyo likiendelea.
Ofisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Jovin Bararata, akizungumza na wakulima wa Kata ya Kibindu.
Mkurugenzi
wa Fedha wa Fedha na Utawala wa COSTECH, Shabani Hussein (wa pili
kulia), akimkabidhi Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kibindu, Juma Athumani
(kushoto), mbegu ya mahindi ya Wema 2109 katika uzinduzi wa shamba
darasa uliofanyika leo katika Kata hiyo Mbwewe mkoani Pwani. Wengine
kutoka kulia ni ni Matifiti Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu, Ofisa
Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Jovin Bararata, Diwani wa
Kata ya Kibindu, Ramadhani Mkufya na Ofisa Kilimo Mkoa wa Pwani,
Kapilima George.
Wanawake wa Kata ya Kibinda wakiwa kwenye uzinduzi wa mbegu hiyo.
Matifiti
Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi
Hamidu, akitoa maelezo ya upandaji wa mbegu hiyo kwa wakulima wa Kata
ya Kibindu.
Diwani wa Kata ya Kibindu, Ramadhani Mkufya , akichangia jambo.
Ofisa Kilimo Mkoa wa Pwani, Kapilima George, akizungumza na wakulima wa Kata ya Kibindu.
Na Dotto Mwaibale, Chalinze
WAKULIMA wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoani wa Pwani wamefurahia kupokea mbegu
bora ya mahindi aina ya Wema 2109 kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na
Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa na Bioteknolojia kwa Maendeleo ya
Kilimo (OFAB) kwa ajili ya kupandwa kwenye mashamba darasa katika
halmashauri hiyo.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano ya mbegu hiyo kwenye uzinduzi wa mashamba darasa
katika vijiji vya Diozile na Kibindu vilivyopo Kata ya Msoga mkoani
humo Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Pwani,Kapilima George alisema mbegu hiyo
itasaidia kuongeza tija ya uzalishaji wa mahindi katika halmshauri hiyo
hivyo amewataka wakulima kuichangamkia.
"Tuwashukuru
COSTECH na OFAB kwa kutuletea mbegu hii ambayo kwetu itakuwa ni
mkombozi mkubwa katika mkoa wetu hasa kwa wakulima wa Kata ya Kibindu
ambao ni vinara kwa kilimo cha mahindi katika mkoa wetu" alisema George.
Alisema
mkoa wa Pwani kwa mwaka jana ulizalisha tani 110 za mahindi huku tani
65 zikizalishwa na Kata ya Kibindu jambo la kuwapongeza wakulima wa kata
hiyo.
Alisema
mbegu hiyo itaongeza msukumo wa kilimo ilimo cha mahindi kwenye
halmashauri hiyo hivyo kujikwamua kupata baa la njaa na ziada kuuza.
Aliwaomba
wakulima hasa kwa wanavikundi waliopata mbegu hizo kuhakikisha
wanayatunza mashamba darasa hayo kwa manufaa ya wakulima wote wa wilaya
hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH wakati wa kukabidhi mbegu hizo, Mkurugenzi wa Fedha wa Fedha na Utawala wa COSTECH, Shabani Hussein alisema
kazi
kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali katika masuala yote yanayohusu
Sayansi na Teknolojia na kusimamia tafiti zote za kisayansi katika
maeneo mbalimbali na kilimo na kuhakikisha zinawafikia walengwa ambao ni
wakulima.
Alisema
mbegu hizo walizozikabidhi zimefanyiwa utafiti na zitapandwa katika
mashamba darasa na baadae kusambazwa kwa wakulima wengine ili kuondoa
changamoto ya kukosekana kwa mbegu bora kutokana na wakulima kukabiliwa
na mbegu ambazo zilikuwa hazina ubora.
Matifiti
Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi
Hamidu alisema iwapo mkulima atafuata ushauri wa upandaji wa mbegu hiyo
ya Wema 2109 katika ekari moja atapata magunia 35 tofauti na mbegu
nyingine ambapo wanapata chini ya hapo.
Aliongeza
kuwa mbegu hiyo italeta matokeo mazuri iwapo kanuni za kilimo bora
zitafuatwa kama vile kufuata vipimo, maandalizi ya shamba, matumizi ya
mbolea zote ya kupandia na kukuzia na kuwa mbegu hiyo ni moja kati ya
mbegu 11 zilizofanyiwa utafiti.
Ofisa
mradi huo kutoka COSTECH, Bestina Daniel alisema kwa mkoa huo wametoa
mbegu kilo 58 kwa ajili ya mashamba darasa katika wilaya ya Bagamoyo na
Chalinze ambapo kwa wakulima mmoja mmoja wametoa kilo 42 pamoja na
mbolea ya kupandia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269