.

MANGULA: VIJANA CHAMA HAKIJENGWI KWA 'SLOGANS', KINAJENGWA KWA KWENDA NDANI NA NJE YA CHAMA KWA KARIBU KAMA KUKU ANAVYOLALIA MAYAI. NDIVYO KURA ZINAVYOPATIKANA

Apr 2, 2018

*Asema, Kazi ya kubuni na kusimamia miradi ni ya Serkali
*Kazi ya CCM nie kuisimamia tu Serkali.
*Atoboa siri, asema miradi ya maendeleo ina tabia ya      kuelimisha wananchi, rika jipya na wanasiasa kufanya harakati.

NA BASHIR NKOROMO
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula amewaambiawana CCM hasa Vijana kuwa kazi ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama siyo yao na kuwapambanuliwa kuwa kazi yao ni kutangaza ubora wa CCM ndani na nje ya Chama kwa sababu kazi ya Utekelezaji wa Ilani ni ya Serikali na kazi ya CCM ni kusimamia tu.

Katika Salam zake za Pasaka kwa Vijana, Mangula amewataka wajue kwamba maendeleo ya miradi ni kitu chema sana, lakini changamoto yake kubwa ni kwamba miradi ya maendeleo ina tabia ya kuelimisha wananchi na rika jipya la wananchi na wanasiasa hivyo kuibua upinzania mkubwa, hivyo wakati serikali inajenga miradi ni lazima wana CCM hasa vijana kuendelea kuwa karibu na wanachama na wasio wanachama kama kuku anayelalia mayai.

Amesema, siyo sahihi Vijana wa Chama kupita wakijipiga vifua kuhusu miradi wakati hawakijengi Chama kwa kutarajia tu kwamba uwepo wa miradi utaifanya CCM kushinda katika Chaguzi mbalimbali ikiwemo za kushika dola.

"Lusekelo (jina kamili halikupatikana), na vijana wenzako wana CCM leo nawapeni ujumbe wa Pasaka, ni salamu kwenu nyote, fanyeni kazi ya Chama, si Miradi au Ujenzi au Mipango ya Serikali itakayowapatia kura hata kama mizuri sana, sana sana itaongeza joto la upinzani. 

Muelewe hivyo uhusiano kati ya Miradi ya Maendeleo na kura ya mtu kwa Chama tawala ni vigumu kupima, na kwa hakika kusimamia utekelezaji wa Ilani kwa kiasi kikubwa ni kusimamia dola itekeleze ahadi za maendeleo zilizo kwenye ilani hiyo na kwa hakika lazima mjue miradi hiyo pia huimarisha upinzani." alisema Mangula

"Dawa ninini, ni kufanya kazi ya Chama nje na ndani ya Umma, na kazi ya Chama ndani ya Chama, msikalie mmbweteka na 'slogans' tuu - kidumu, zidumu, kidumu Chama cha Mapinduzi, mtapigwa bao tena kwa fitina yenu wenyewe, ubinafsi wenu, makundi na kutaka vyeo ili 'kupiga'.

"Someni historia ya vyama vikubwa vilivyoanguka, Chama Cha Kikomunisti cha Urusi (USSR ) na sera zao za maendeleo, War communism, halafu New Economic Policy ikafutia Stalinism.  ni kweli USSR ilijenga maendeleo na Urusi kuwa Taifa kubwa duniani lakini kwa kuwa walisahau kazi ya Chama, wateule wachache wakawa Chama, msukosuko uliotokea vikasambaratika vyote Chama na Taifa", alisema Mangula.

Alisema, "miradi ya maendeleo ina tabia ya kuelimisha wananchi na rika jipya la wananchi na wanasiasa: nitakupeni mfano toka 2005 tulipopata 80% na kidogo ya kura sera yetu shule kila kata,  barabara kuunganisha mikoa lami na fikiria UDOM tukaanzisha sisi halafu tukakalia 'iena iena CCM nambari one' bila kufanya kazi ya Chama - UDOM ikawa ndiyo kambi ya wapinzani, na kwa hakika kura zetu zilikatwa kwa asilimia 30, kama hatuoni na kwa hakika uchaguzi ni 50/50 itategemea kazi ya Chama na pia aina ya mgombea".

 Mangula alisema sababu nyingine ya msingi wana CCM wamekalia mipasuko na kufanya kazi za dola  kwa kuona huko ndiko 'kunalipa'. " msaidieni Mwenyekiti kura ingawa inachangiwa na miradi lakini ili uipate ni lazima umfikie mwananchi, ni imani kama sala hujengwa kuna ijumaa/Jumapili ngapi kwa mwaka waumini wanakutana kuaminishwa jambo lile lile - Mungu yupo? Kazi ya Chama ndani na nje ni ya kudumu kuwaaminisha watu kama CCM inachagulika kwa sababu Itikadi, imani na siasa yake ya Ujamaa na Kujitegemea inawajali wanyonge na kwa sababu. lakini kukalia. Kidumu Chama Tawala, tutapigwa", alisema Mangula.

Alisema "maendeleo mengi elimishi mijini na vijijini huwafungua vijana na wananchi kutafuta mabadiliko pamoja na ya siasa. Tathmini 2010 ilitufungua macho majimbo zaidi ya kumi kati ya 28 ya makao makuu ya mikoa, ubunge ulienda upinzani kwa mara ya kwanza, na au tofauti ya kura kati ya mgombea wa CCM na upinzani ilikuwa ni ndogo, lakini bado tukaendelea 'business as usual', makundi ya kupiga ubinafsi, Kidumu Chama Tawala, Wallah tutapigwa katika sanduku la kura na hatutarudi tena maana uzoezfu wa kihistoria umeonyesha hivyo, mangula alimalizia salam zake kwa kusema " hiyo ndiyo salamu yangu ya Pasaka kwa wana CCM wenzangu - MUNGU AKUBARIKI

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช