Breaking News

Your Ad Spot

Apr 29, 2018

RAIS DK. MAGUFULI AFUNGUA SEHEMU ILIYOKAMILIKA YA KILOMETA 189, KATI YA IRINGA-MIGORI-IFUFU KWA KIWANGO CHA LAMI, KATIKA BARABARA YA IRINGA-DODOMA, LEO.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Jeremy Aguma wa pili kutoka kulia  wakivuta utepe kwenye jiwe la msingi kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami. Sherehe hizo za ufunguzi zilifanyika katika kijiji cha Ndolela kilichopo Isimani nje kidogo ya mji wa Iringa
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwakilishi wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB Jeremy Aguma, Balozi wa Japan Masaharu Yoshida wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa , Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na viongozi wengine wa Serikali na wageni kutoka nje ya nchi. 
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa jukwaa kuu pamoja na Balozi wa Japan Masaharu Yoshida, Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi, pamoja na Waziri wa Mambo ya nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga wakifatilia sherehe za ufunguzi wa barabara ya ya Iringa-Dodoma katika sehemu ya Iringa-Migori-Fufu Km 189 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Iringa mjini waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili akitokea Isimani mkoani Iringa
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Iringa mjini waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili akitokea Isimani mkoani Iringa
Mwananchi wa Iringa mjini akipuliza pembe ya ng’ombe  wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili Iringa mjini katika ziara ya kikazi. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages