.

RAIS DK. MAGUFULI APOKEA NDEGE MPYA YA BOMBARDIER Q400, AWEKA JIWE LA MSINGI USIMIKAJI WA MFUMO WA RADA KATIKA VIWANJA VINNE VYA NDEGE NCHINI

Apr 2, 2018

 Rais Dk. John Magufuli akipunga mkono kwa furaha kuwashukuru wananchi  wakati akiingia katika ndege mpya ya Bombardier Q400 ilipowasli na kufanyiwa mapokezi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo ikitokea nchini Canada
 Rais Dk. John Magufuli akionyesha wananchi  wakati akiingia katika ndege mpya ya Bombardier Q400 ilipowasli na kufanyiwa mapokezi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, leo ikitokea nchini Canada
 Rais Dk. John Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli, viongozi mbalimbali wa dini, Serikali na wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakati akikata utepe kuzindua Ndege mpya ya Shirika la ndege la ATCL aina ya Bombardier Q400, baada ya ndege hiyo kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
 Rais Dk. John Magufuli akiwainua mikono marubani waliowasili na ndege mpya ya Bombardier Q400, kutoka nchini Canada, baada ya Ndege hiyo kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Rais Dk. John Magufuli akiweka jiwe la msingi mfumo wa usimikaji wa Rada katika viwanja vinne vya ndege  vya Uwanja wa Ndege wa Kimafaifa wa Julius Nyerere wa jijini dar es Salaam, Mwanza, KIA wa Kilimanjaro na Songwe katika hafla iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam


HAFLA YAMKUTANISHA RAIS NA DIAMOND PLATINUM
 Rais Dk. John Magufuli akimsikiliza mwanamuziki wa Bongo flavor Naseeb Abdul, maarufu kwa jina la Diamond Platinum, alipoonana naye baada ya kuweka jiwe la msingi Mfumo wa Usimikaji wa Rada katika viwanja vinne vya ndege vya Julius Nyerere-Dar es Salaam, Mwanza, KIA-Kilimanjaro na Songwe katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais Dk. John Magufuli akifurahia jambo na mwanamuziki wa Bongo flavor Naseeb Abdul, maarufu kwa jina la Diamond Platinum, alipoonana naye baada ya kuweka jiwe la msingi Mfumo wa Usimikaji wa Rada katika viwanja vinne vya ndege vya Julius Nyerere-Dar es Salaam, Mwanza, KIA-Kilimanjaro na Songwe katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª