Breaking News

Your Ad Spot

May 5, 2018

RC RUVUMA AFANYA ZIARA Y A KUSTUKIZA NA KUMBAMBA MTU AMBAYE AMEANZISHA UCHIMBAJI WA MADINI KATIKATI YA MTO MUHWESI WILAYANI TUNDURU

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme amefanya ukaguzi wa kushitukiza katika kijiji cha Muhuwesi Wilayani Tunduru akiwa na Kamati zote za ulinzi na usalama mkoa na wilaya na kugundua uwepo wa  Mchimbaji anayejenga vibanda na kambi kubwa inayotarajia kujishulisha na uchimbaji pamoja na uwepo wa  mitambo kwa ajili ya kuanza kuchimba madini mbalimbali katikati ya Mto Muhuwesi

 RC Mndeme amesena kitendo hicho ni uvunjifu wa sheria ya Hifadhi ya Maji no 11 ya mwaka 2009 kifungu cha 34 ,na uharibifu wa Mazingirana kuelezea kuwa kuchimbwa madini katika eneo hili kutasababisha uchafuzi wa maji ya Mto Ruvuma na kuharibu mfumo wa usimamizi na upimaji wa maji  katika bonde la mto Ruvuma

 RC MNDEME amesisitiza kuwa kuchimbwa kwa madini katika ENEO Hilo kutasababisha kuharibika kwa daraja lililojengwa na Serikali kwa ajili ya barabara ya Mtwara Corridor kuwa eneo hilo linamwamba mgumu.

 Barabara hiyo ni muhimu kwa Uchumi wa Wananchi wa Mkoa wa Ruvumana Taifa kwa ujumla kwa sababu wameiomba barabara hii kwa muda mrefu na Serikali kujenga kwa maendeleo endelevu ya wananchi wake.

RC MNDEME amemwagiza Kamishina wa Madini Kanda ya Nyasa kufuta Leseni aliyotoa kwa Mchimbaji na kumtaka Ndugu Yassin Musa Salum na wenzake  kuondoka katika eneo hilo na kuondoa mitambo yao ndani ya siku saba(7) baada ya hapo watachukuliwa hatua kali.

Aidha Amemtaka Afisa Bonde la Ruvuma aliyopo Mkoani Ruvuma kulinda eneo hilo pamoja na vifaa vinavyotumia katika upimaji maji vilivyowekwa na serikali kwa malengo ya kujua ujazo wa maji katika Bonde la mto Ruvuma na Mtwara kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages