Breaking News

Your Ad Spot

Apr 19, 2025

JK AWASILISHA SALAMU ZA RAIS SAMIA KWA KIONGOZI WA BURKINA FASO KEPTENI TRAORE

Rais Mstsaafu wa Awamu ya Nne na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kiongozi wa Burkina Faso Kepteni Ibrahim Traore mjini Ouagadougou na kushuhudiwa na baadhi ya maafisa waandamizi wa nchi zote mbili.


Mhe. Kikwete aliwasilisha pia salamu za Rais Samia ambazo zilielezea umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano wa kijamii na kiuchumi kama njia muhimu kwa bara hilo kujitegemea, hususan katika kipindi hiki ambapo misaada kutoka nchi za magharibi imepungua kwa kiasi kikubwa.

Rais Mstaafu pia alitumia kumtambulisha kiongozi huyo mgombea wa Tanzania katika nafasi ya  Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Profesa Mohamed Janabi.











No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages