Na Bashir Nkoromo, theNkoromo Blog
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Beach A, Kata ya Kawe Jijini Dar es Salaam, Esther Mwamyalla, katika juhudi zake kuhakikisha wananchi katika maeneo yote ya Mtaa huo wanaishi kwa amani na usalama pamoja na mali zao, ameendelea kuweka mkazo kuhakikisha kila mwananchi anashiriki moja kwa moja au kuchangia fedha kwa ajili ya Ulinzi Shirikishi.
Mwamyalla amekuwa akifanya hivyo tangu alipochaguliwa kwa kishindo katika uchaguzi uliliofanyika hivi karibuni, ikiwa ni mojawapo ya jukumu lake kwa mujibu wa sheria za Manispaa ya Kinondoni ambamo Mtaa wake umo.
Ili kutimiza jukumu hilo, amekuwa akitumia mbinu mbalimbali ikiwemo kushirikiana na wadau mbalimbali likiwemo Jeshi la Polisi (Polisi Kata), kutoa elimu kwa wananchi wake juu ya faida na umuhimu wa kila mmoja kushiriki Ulinzi huo Shirikishi. Msikilize hapa akitoa elimu hiyo👇
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269