Breaking News

Your Ad Spot

Jan 12, 2010

KILELE CHA MIAKA 46 YA MAPINDUZI ZANZIBAR LEO

 WATANZANIA leo wanaadhimisha miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoung'oa utawala wa kisultani na doila kushikwa na wazalendo chini ya Jemedari, Mzee Abeid Amani Karume (pichani-kulia). Rais wa Zanzibar (kushoto) Amani Abeid Karume (Simba Mtoto), ndiye atakuwa mgeni rasmi katika shamrashamra zitakazoambatana na paredi ya JWTZ,Polisi na KMKM kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.


RAIS wa Zanzibar, Amani Abedi Karume akikagua gwaride lilioandaliwa kusherehekea miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar, leo katika  Uwanja wa Gombani, Pemba (picha kwa hisani ya Mdau kutoka ofisi ya makamu wa Rais-Clerance Nanyaro


WANACAMA wa Chama cha Waendesha pikipiki Zanzibar wakishiriki katika maandamanao hayo.
ASKARI  walioshuriki gwaride katika sherehe hizo wakitoa heshima kwa Rais wa Zanzibar. WAZIRI Kiongozi mstaafu, Dk.Mohamed Ghalib Bilal, na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad ambaye amewahi pia kuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar, wakiwa katika sherehe hizo.

RAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume akisalimiana na Waziri Kiongozi wa zamani wa Zanzibar, Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad katika shamra shamra hizo.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages