Breaking News

Your Ad Spot

Jan 13, 2010

MATATANI KWA NYAVU ZENYE MATUNDU MADOGO



MFANYABIASHARA mwenye asili ya Kiasia,Salum Gulam Hussein akiwa chini ya ulinzi wa polisi akipofikishwa Mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, kujibu mashitaka ya kupatikana na nyavu zenye matundu ya chini ya inchi tatu kinyume cha sheria.

MAELEZO YA MASHTAKA

fULL STOPRy

                                                               NA NJUMAI NGOTA

MSIMAMIZI wa Kampuni ya Uvuvi ya Imara na mfanyabiashara, jana walipandishwa kizimbani kwa mahakimu wa wawili kwa mashitaka tofauti.

Washitakiwa hao, mmoja anadaiwa kuwazuia maofisa kufanya kazi zao na mwingine kupatikana na nyavu za uvuvi kinyume cha sheria.

Mawakili wa serikali wakiwasomea mashitaka mbele ya mbele ya mahakimu wawili wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambao ni Victoria Nongwa na Devota Kisoka .

Washitakiwa hao ni Bushiri Oyala (47) na Salimu Hussein (61). Wakazi wa Dar es Salaam.

Katika shitaka linalomkabili Oyala lililopo mbele ya hakimu Victoria, anadaiwa Januari 8, mwaka huu, saa 6.00 mchana katika Kampuni ya Uvuvi ya Imara, Temeke, aliwazuia maofisa wa polisi kufanya kazi zao.
Mashitakiwa alikana shitaka ambapo upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili wa serikali Monica Mboga, ulidai upelelezi bado haujakamili na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hata hivyo, alitaka kuiomba mahakama hiyo kuharibu nyavu hizo alizokamatwa nazo mshitakiwa, Hakimu alisema wafanye marekebisho ya hati hiyo kwanza.

Katika shitaka linalomkabili Hussen lililopo mbele ya Hakimu Devota, anadaiwa Januari 9, mwaka huu, saa 4.00 asubuhi, katika duka la kampuni hiyo, wilayani Ilala, alipatikana na nyavu zenye thamani ya sh. 945,000.

Mshitakiwa alikana shitaka hilo ambapo mwendesha mashitaka Emma alidai upelelezi bado haujakamilika, hata hivyo aliiomba mahakama hiyi itaifishe nyavu hizo.

Wakili wa upande wa utetezi, Gaudiousus Ishengoma anayemtetea mshitakiwa huyo alipinga ombi hilo. Hakimu alisema atalitolea uamuzi Januari 28, mwaka huu.
ciao.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages