Breaking News

Your Ad Spot

Feb 26, 2010

KATONI 13,036 ZA ALYWAS FEKI ZA MILIONI 1295.54 ZATEKETEZWA DAR

Alyws bandia

Vijana wakizisambaza katoni za pedi  bandia tayarai kuzichoma

Always bandia zikiteketea kwa moto

                                                                      Story
TUME ya Ushindani Nchini (FCC), imeteketeza katoni 13,036 za Pedi feki za sh. Milioni 195.5, leo kwenye dampo la Pugu Kinyamwezi, Dar es Salaam.
     Akizungumza na waandishi wa habari, ofisa uhusiano wa FCC, Frank Mdimi alisema Pedi hizo zimekamatwa katika miji ya Arusha na Dar es Salaam. kati ya Januari na Februari, mwaka huu na zinatoka nchini China kwa kuingizwa nchini na wafanyabiashara watano aliowataja kuwa ni  Mazeh Meghji ambaye alikamatwa na katomi 2,882, za sh. milioni 43.2, Elibariki Mollel katoni 1,221, za sh. Milioni 16.8, Gabriel Massawe katoni 253 za sh. Milioni 3.7.
    Wengine ni Ally Gulamali, katoni 570 za sh. Milioni 8.5, wote kutoka Dar es Salaam na Paulo Lema kutoka Arusha ambaye alikamatwa na katoni 8,110 za sh. Milioni 121.6.
    Mdimi alisema Pedi hizo zina madhara mengi kwa watumiaji ikiwa ni pamoja na kusababisha ukurutu au fangasi sehemu za siri.
    Aliwaomba wananchi kuwa makini wanaponunua bidhaa na iwapo wata kuwa na wasiwasi na bidhaa yoyote watoe taarifa kwenye vyombo vinavyo husika.
          Mdimi alisema jukumu la kukamata na kuwafichua waingizaji wa bidhaa bandi si la FCC pekee bali linahitaji ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages