Breaking News

Your Ad Spot

Feb 13, 2010

BAADA YA KUTEMWA NA MAHAKAMA YA RUFANI, WATOTO WA BABU SEYA WASHAURIWA KUTODAI FIDIA

BAADA ya kuokolewa kwa rufani kutoka katika kifungo cha maisha, watoto wa Babu Seya, Nguza Mbangu na Francis Nguza wameshauriwa  kuIdai fidia Serikali
   Akizungumza na Kituo cha Luninga cha hapa nchini cha Mlimani TV,  wakili aliyesimamia rufani hiyo, Mabere Marando alisema asingewashauri vijana hao kuomba fidia kwa sababu kuna uwezekano mkubwa wakashindwa na hivyo kulazimika wao kulipa gharama.
   Marando alisema, hiyo ni kwa sababu kwa alivyoiona kesi yenyewe ni kwamba vijana hao hawakupelekwa mahakamani kukiwa hakuna kesi ya kujibu, kwa kuwa ukweli ni kwamba tukio la ubakaji inaonekana lilifanyika isipokuwa kuhusu ni nani hasa walihusika ndiyo ilikuwa hakuna usahihi.
  "Hawa wangeweza kudai fidia kama ingekuwa inaonyesha dhahiri kwamba hakukuwa na kesi dhidi yao ya kujibu mahakamani... lakini ni kwamba kesi ya kujibu ilikuwepo isipokuwa nani alihusika ndiyo ilikuwa tatizo", alisema Marando.
  Alisema, kwa sasa hatua uamuzi uliochukuliwa na hamakama ya rufani wa kuwaacha huru Nguza Mbangu na Francis Nguza  na kuwaamuru kuendelea kutumikia hukumu ya awali ya kifugo cha maisha  babu Seya na mwanye Papii Kocha ni ya mwisho kwa mujibu wa taratibu za sheria za hapa nchini.
   Takriban miaka sita iliyopita, Babu Seya, Papii Kocha, Francis Nguza na Nguza Mbangu walihukumiwa na mahakama kuu kutumikia kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kulawiti na kubaka nyumbani kwao Sinza jijini Dar es Salaam.
    Baada ya kukata rufani, Almahisi wiki hii, rufani hiyo ilitolewa uamuzi ambao uliwaacha huru wawili huku Babu seya na Papii Kocha wakiamriwa kuendelea kusota gerezani.
NGUZ Mbangu
Francis Nguza
Babu Seya na Papii Kocha baada ya rufani hiyo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages