RAIS Jakaya Kikwete na mwenyeji wake Raıs wa Uturuki Abdukkah Gul wakıkagua gwaride la heshima muda mfupi baada ya Rais Kıkwete kuwasili katika ikulu ya nchı hıyo iliyopo jijini Ankara leo asubuhi.
Rais wa Uturuki Abdullah Gul na mkewe wakiwakaribisha ikulu ya jıjını Ankara JK Mama Salma leo asubuhi
RAIS Jakaya Kikwete akifafanua jambo wakati wa mkutano n a waandishi wa habari mara baada ya kufanhya mazungumzo rasmı katıka ikulu ya Ankara nchını Uturukı leo asubuhi.Pembenı akımsıkılıza nı Rais wa nchı hiyo Abdullah Gul.Raıs Kıkwete yupo katıka zıara ya kikazi nchini Uturuki (Pıcha na mdau Freddy Maro).
STORY
Na Mwandishi Maalum
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo 18 Feb, 10 anaanza ziara ya siku tatu nchini Uturuki kwa makaribisho rasmi ambapo Rais wa Uturuki Mheshimiwa Abdullah Gul atamkaribisha Rais Kikwete katika kasri ya nchi hiyo.
Mara baada ya makaribisho hayo, viongozi hao wawili watafanya mazungumzo rasmi ya kiserikali na kushuhudia utiaji saini kwa mikataba mitano kati ya nchi mbili hizi shughuli ambazo zitafanywa na mawaziri.
Mchana wa leo, (18.2.10) Rais na ujumbe wake utakutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyid Erdogan kabla ya kukutana na kufanya mazungumzo na spika wa Bunge la Uturuki Mheshimiwa Mehmet Ali Sahin.
Rais Kikwete pia atakutana na kufanya mazungumzo na Umoja wa Wafanyabiashara wa Uturuki na baadaye kukutana na mabalozi wa Nchi za Afrika waliopo Uturuki na baadaye jioni hii Rais Kiwete na ujumbe wake watahudhuria dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269