Breaking News

Your Ad Spot

Feb 5, 2010

TOT PLUS YAKABIDHIWA VYOMBO VIPYA VYA MUZIKI LEO

KATIBU wa NEC ya CCM, Uchumi na Fedha, Amos Makalla akipiga tumba wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya muziki kwa Kundi la Tanzania One Theatre (TOT Plus), kwenye Ofisi ya CCM Mwananyamala Mwinjuma ,Ddar es Salaam, leo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TOT Plus, kapteni John Komba ambaye pia ni Mjumbe wa NEC-CCM. Na wengine kuhsoto ni meneja wa Bandi ya TOT Plus Kig Dodoo La Bouche na Mwanamuziki wa kundi hilo, Khadija Kopa.
KATIBU wa NEC ya CCM, Uchumi na Fedha, Amos Makalla akipiga drams wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa vya muziki kwa Kundi la Tanzania One Theatre (TOT Plus), kwenye Ofisi ya CCM Mwananyamala Mwinjuma ,Dar es Salaam, leo. Kushotoa ni Mkurugenzi Mtendaji wa TOT Plus, kapteni John Komba  na kulia ni Meneja wa TOT Plus, King Dodoo La Bouche
BAADHI ya wanamuziki waliokuwa kwenye sherehe hizo
KIONGOZI wa nidhamu wa bendi ya TOT Plus, Mwimbaji mahiri wa bendi hiyo Abdul Misambano akijaribu kuimba kwa kutumia kinasa sauti ambacho ni miongoni mwa vyombo hivyo.
WANENGUAJI Roya Ngolo, Hadija POmari aka Tshalamwana na  Jumbe Ngeoda wakifurahi baada ya makabidhiano ya vyombo hivyo.
Rapa Josephat Mbarouk aka Jua kali na mwimbaji ......wakila pozi baada ya bendfi kukabidhiwa vyombo hivyo leo

STORY

KUNDI la Tanzania One Theatre (TOT Plus) limetakiwa kuvitumia vyombo vyake vipya vya muziki kuonyesha kuonyesha umahiri wake zaidi katika fani zake mbalimbali za burudani kwa mashabiki wake.

Kauli hiyo ilisemwa na Katibu wa NEC ya CCM Uchumi na Fedha, Amos Makalla alipokuwa akikabidhi vyombo vipya kwa kundi hilo, leo katika ukumbi wa CCM Mwinjuma, mwananyamala mjini Dar es Salaam.
   Makalla alisema, vyombo hivyo ambavyo vimenunuliwa na CCM kwa sh. milioni 100, viwe chachu ya kufanya kundi hilo kug'aa zaidi katika fani za muziki wa dansi, ngoma za asili, kwaya na taarab, badala ya kudidimia na kupoteza mashabiki.

Aliwataka wanamuziki na viongozi wa kundi hilo, kuwa wabunifu kwa kuwa vyombo ambavyo limepewa kundi hilo vina uwezo wa kuwawezesha kufanya lolote katika kuuboresha muziki.

Mkurugenzi wa TOT Plus John Komba alisema, vyombo hivyo vitatumiwa na kundi katika fani zote za burudani kinazofanya, na pia mbali na kwenye maonyesho vyombo hivyo ni mahsusi kwa kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages