WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Profesa Mark Mwandosya akimkabidhi funguo za gari, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Rorya mkoani Mara, Ernest Basaya ikiwa ni ishara ya kumkabidhi mgawo wa gari moja kwa Halmashauri hiyo, Halmashauri 61 za wilaya, zilipokabidhiwa kila moja gari, kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya sekta ya Maji nchini, leo makao Makuu ya wizara hiyo Ubungo mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Mbunge wa Rorya Profesa Philemon Sarungi.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya maji na Umwagiliaji Christopher Sayi (kushoto), akibadilishana mawazo na mkuu wake, Waziri wa wizara hiyo, Profesa Mark Mwandosya, katika sherehe ya wizara hiyo kuzikabidhi Halmashauri 61 za wilaya gari moja kila Halmashauri kwa ajili ya kusaia utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya sekta ya Maji nchini, leo makao Makuu ya wizara hiyo Ubungo mjini Dar es Salaam. BAADHI ya magari kati ya 61 ambayo Wizara ya Maji na Umwagiliaji ilikabidhi kwa Halmashauri 61 za wilaya, ambapo kila Halmashauri imepata moja kwa ajili ya kusaia utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya sekta ya Maji nchini, leo makao WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Profesa Mark Mwanmdosya akijaribu gari moja kati ya 61 ambayo Wizara ya Maji na Umwagiliaji ilikabidhi kwa Halmashauri 61 za wilaya, ambapo kila Halmashauri imepata moja kwa ajili ya kusaia utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya sekta ya Maji nchini, jana makao Makuu ya wizara hiyo Ubungo mjini Dar es Salaam.
FULL STORI
WIZARA ya Maji na Umwagiliaji leo imezikabidhgi Halmashauri 61 za wilaya kila moja gari moja kwa ajili ya utekelezaji wa Programu ya sekta ya Maji nchini.
Kabla ya kuklabidhi magari hayo,Katibu Mkuu wa Wizara, Injinia Christopher Sayi alisema, magari hayo ni kati ya 186 yaliyokusudiwa kupelekwa kwenye Halmashauri nchini, na kwamba Wizara unatarajia kupokea mengine 125 mwishoni mwa mwezi huu ili kutosheleza kabisa mahitaji ya taasisi za utekelezaji wa Programu hiyo ya maji nchini.
Pamoja na magari hayo aina ya Toyota land Cruiser, Wizara ilikabidhi pia mashine 56 za kurudufu, yaani Scanner kwa Halmashauri zilizokwishapata Printer awamu iliyopita.
Kwa mujibu wa Sayi alisema ili kuzijengea uwezo Taasisi za utekelezaji wa programu ya maji katika ngazi za chini ikiwa ni pamoja na Halmashauri, Mamlaka za maji Mijini na Bodi za Maji za Mabonde, Mwezi Novemba mwaka jana na Januari mwaka huu taasisi hizo zilipewana serikali vitendea kazi.
Baadhi ya vitendea kazi hivyo vikuwa Pikipiki 252 na mashine za uchapaji viulivyotolewa kwa Halmashauri 111, pikipiki 120 kwa mamlaka zaMaji Mijini, Pikipiki 35,Mtumbwi wa kupima maji.
Halmnashauri 61 zilizokabidhiwa magari leo Mwanza ni Geita, Magu, Jiji la Mwanza, Sengerema, Kwimba, Misungwi na Ukerewe, Shinyanga ni Bariadi, Shinyanga,Manispaa ya Shinyanga,Maswa, Kahama, Meatu, Kishapu na Bukombe, Kagera ni Biharamulo, Manispaa ya Bukoba, Bukoba, Karagwe, Misenye, Muleba, Chato na Ngara, Mara ni Bunda, Manispaa ya Musoma. Musoma, Serengeti, Tarime na Rorya. Tabora ni Igunga, Sikonge, Nzega, Tabora, Urambo na Tabora/Uyuwi. Rukwa ni Halmashsuri ya Mji wa Panda, Mpandsa, Nkasi, Sumbawanga na Manispaa ya Sumbawanga.
Kigoma ni Halmashauri za Kasulu, Kibondo, Manispaa ya Kigoma Ujiji na Kigoma. Manyara ni Halm,ashsuri ya Hanaang, Mbulu, Babati, Mji wa Babati, Kiteto, na simanjiro. Mtwara ni Halmashauri ya Nanyumbu.Menya ni Halmashauri ya Ileje, Mbeya, Rungwe, Chunya, Kyela, Mbozi, Mbarali, na mji wa Mbeya na Arusha ni Halmashauri ya Ngorongoro.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269