Mjane wa aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana , ambaye kuuwawa kwake kulikuwa chanzo cha mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda amekamatwa nchini Ufaransa.
Agathe Habyarimana (pichani) amekuwa akilaumiwa na serikali ya Rwanda kwa kuhusika katika kupanga mauaji hayo ya halaiki na tangu wakati huo amekuwa akitafutwa na vyombo vya sheria.
Habyarimana, ambaye amekuwa akiishi nchini Ufaransa kwa miaka kadhaa anakanusha madai hayo.
Zaidi ya watu 800,000 kutoka kabila la waTutsis na waHutu wenye msimamo wa wastani waliuwawa katika ukatili huo wa mwaka 94.
Maafisa nchini Ufaransa wanasema Bi Habyarimana alikamatwa mjini Paris na Polisi wanaotekeleza hoja ya kimataifa ya kukamatwa kwake iliyotolewa na Rwanda.
Kukamatwa kwake kunafuatia ziara ya rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy nchini Rwanda wiki iliyopita, ambapo alikiri makosa ya Ufaransa katika mauaji hayo ya mwaka 94.
Rais Habyarimana alifariki Aprili mwaka 94 wakati ndege yake iliporushiwa kombora karibu na uwanja wa ndege wa Kigali.
http://www.bbcswahili.com/
Your Ad Spot
Mar 2, 2010
Home
Unlabelled
MJANE WA HABYARIMANA AKAMATWA UFARANSA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA KIMBARI
MJANE WA HABYARIMANA AKAMATWA UFARANSA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA KIMBARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269