Breaking News

Your Ad Spot

Apr 3, 2010

BONANZA LA MICHEZO LA WATUMNISHI IKULU YA JK NA YA KARUME LAFANA DAR

HABARI KATIKA PICHA
MSHAMBULIAJI wa timu ya Ikulu ya Zanzibar, Salehe Hamadi (kushoto) akipambana na Harison Edward wa timu ya Ikulu ya Dar es Salaam, timu hizo zilipomenyana leo kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu Cha Ualimu (DUCE) Chang'ombe, Dar es Salaam, katika tamasha la michezo la Ofisi hizo. Ikulu ya Dar es Salaam, ilifungwa mabao 3-1. MCHEZAJI wa Ikulu ya Dar es Salaam, Hamis Ndege (kushoto) akijaribu kumthibiti Mohamed Edward wa timu ya Ikulu ya Zanzibar,hizo zilipomenyana jana kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu Cha Ualimu (DUCE) Chang'ombe, Dar es Salaam, katika tamasha la michezo la Ofisi hizo.Mashabiki wa timu ya soka  ya Zanzibar wakishangilia baada ya timu yaokuibuka na ushindi baada ya mechi hiyoMashabiki na wachazaji wa michezo mingine wa timu ya Ikulu ya Dar es Salaam, wakifuatilia mpambano huo wa sokaMchezaji wa netiboli wa timu ya Ikulu, dada nanihiiiii akifuatilia pia soka hilo.Hawa ni kina dada wa timu ya netiboli ambao hawakuamini macho yao baada ya timu yao ya soka kutunguliwa mabao 3-1 na WazanzibarTimu ya kuvuta kamba ya Zanzibar ya wanaume ambayo ilitupwa kwa mbali na ile ya Ikului ya Dar ambayo ilipambana nayo katika mchezo huo.Wavuta kamba wa Ikulu ya Zanzibar wakigaragazwa na wenzao wa DarMkurugenzi wa huduma za Ikulu ya Dar es salaam, Frank Mganga akiipongeza timu yake baada ya kuwashinda wenzao wa zanzibar katika mashindano ya kuvuta kamba.TIMU za neboli za Ikulu ya Dar na ile ya Zanzibar wakichuana  kutafuta nani mbabe ambapo baadaye ilibainika ile ya Dar ni zaidi baada ya kuwabwaga wenzao mabao 22-14Hamis Mnyupe na Roman Mng'ande wakipuliza saxaphone wakati bendi yao ya Msondo ilip[okuwa ikitumbuiza kwenmye bonanza hilo kwenye viwanja vya DUCE Chan'gombe Dar es Salaam.MKURUGENZI wa Huduma za Ikulu, Ofisi ya Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano katika Bonanza hilo, Frank Mganga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu lengo la michezo hiyo kwa wafanyakazi wa Ikulu. Kushoto ni Mnikulu ya Ikulu ya Zanzibar Shabani Hiliki.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages