MWANDISHI wa habari wa Uhuru Publications Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Uhuru,Mzalendo na Burudani, Selina Wilson akipokea kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Clement Mshana, cheti cha kuhitimu mafunzo ya uandishi wa habari za saratani, katika sherehe ya kutunuku vyeti hivyo, jana katika ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) mjini Dar es Salaam. MKURUGENZI wa Idara Habari (Maelezo), Clement Mshana akimkabidhi cheti mtayarishaji wa vipindi vya afya Mlimani Tv, Tuma Dandi, kwa kuwa mshindi wa kwanza katika utayarishaji wa vipindi kuhusu ugonjwa wa Saratani, katika sherehe zilizofanyika jana, katika ukumbi wa Maelezo, Dar es Salaam. JUMLA ya Waandishi wa habari 24, wamekabidhiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo ya uandishi wa habari za saratani, ambayo yaliendeshwa na Chama Cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) kwa kushirikiana na Chama Cha Afya ya Jamii (TPHA) kwa ufadhili wa Chama cha Kimataifa cha saratani Marekani. Pichani Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Clement Mshana (katikati mwenye suti nyeusi) akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu hao baada ya kuwakabidhi vyeti jana, katika sherehe iliyofanyika kwenye ukumbi wa Maelezo mjini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA ABRAHAM NYANTORI - MAELEZO.
Your Ad Spot
Apr 3, 2010
Home
Unlabelled
WAANDISHI WALIOPATA MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI ZA SARATANI WAPATA VYETI LEO
WAANDISHI WALIOPATA MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI ZA SARATANI WAPATA VYETI LEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269