UHAKIKA wa kutimia ndoto ya miaka mingi ya watu kuweza kusafiri kwa teksi na kwa muda mfupi kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, inaelekea kutimia kufuatia kusalia kilometa 20 tu kuifanya barabara hiyo yenye jumla ya kilometa 1,113 kuwa ya lami.
Hatua hiyo inafuatia kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya Dodoma-Manyoni lenye urefu wa kilometa 126, ambayo ilizinduliwa rasmi juzi mjini Manyoni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda .
Katika uzinduzi huo, Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa alimwambia Waziri Mkuu kwamba eneo lililobaki la kilometa 20 ni sehemu ya barabara ya Manyoni-Isuna yenye urefu wa kilometa 55 inayojengwa na kampini ya China Geo Engineering ambayo linatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu.
“Mheshimiwa waziri Mkuu na ndugu wananchi, naweza kusema kwamba sasa ile ndoto iliyokuwa ikisemwa amara kwa mara na Waziri mwenzangu wa Miundombinu aliyetangulia bwana Magufuli itafikia wakati mtu anatoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa teksi inakaribia kutimia kwa kuwa tumebakiza mkia kuifanya barabara ya eneo hilo kuwa ya lami yote”, alisema Kawambwa.
Alisema, barabara ya Dodoma-Manyoni yenye urefu wa kilometa 126 ambayo ujenzi wake umegharibu kiasi cha sh. Bilioni 143, ulianza mwaka 2003 ukifanywa na kampuni ya Konoike ambayo baadaye ilinyang’anywa kazi hiyo baada ya kushindwa kukidhi utendaji na ikapewa kampuni ya ESTIM ya Kitanzania Februari 2009 ambayo imekamilisha ujenzi wote.
Alisema eneo la barabara ya Manyoni-Isuna kwa mujibu wa mkataba linatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu, lakini kulingana na mjenzi wa barabara hiyo, kampuni ya Geo Engineering ya China huenda ikakamilika mwezi Oktoba mwaka huu.
Dk. Kawambwa alisema akwa sasa eneo imejengwa kwa kuzingatia viwango na mahitaji yote ya watuamiaji wa barabara ikiwemo kuwekwa maeneo ya waenda kwa miguu, alama za barabarani na njia za waendesha baiskeli kwa maeneo yanayohitajika.
Alisema, pamoja na kuweza kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa teksi na kwa mwendo mzuri zaidi kufuatia kukamilika kwa barabara ya Dar es Salaam hadi Mwanza, pia karibu itawezekana kufanya hivyo kutoka Mtwara hadi Mwanza kufuatia kukaribia kukamilika barabara za Mbwemkulu-Mingoyo (Kilometa 95), Nangurukuru-Mbwemkulu(km95) na Somanga –Matandu (kilometa 33).
Hata hivyo, Dk. Kawambwa alieleza kusikitishwa kwake na baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakiharibu au kuiba mioundombinu ya barabara i8kiwemo alama za barabarani, akitoa mfano kwa wizi wa lama za barabarani uliofanywa na baadhi ya wananchi katika eneo la Chikuyu , Dodoma-Manyoni.
Kufuatia maelezo hayo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameagiza wakuu wa mikoa na watendaji wote wenye dhamana, kuhakikisha wanaweka udhibiti wa kuhakikisha inakomeshwa tabia ya baadhi ya watu kuhujumu miundombinu ya barabara kwa kuiba alama za usalama barabarani na kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo za kilimo kwenye eneo la hifadhi za barabara.
Waziri Mkuu aliwataka watendaji hao kusimamia kwa karibu ili kuhakikisha wananchi hawalimi hadi ndani ya mita 25 kutoka kwenye barabara kwa mujibu wa sheria na kuwataka kuchukua hatua za kisheria kwa watakaobainika.
“Nawaagiza wakuu wa mikoa na watendaji wote, hebu shughulikieni kwa dhati kuhakikisha udhibiti wa hawa wanaaoiba na kufanya shughuli za kilimo katika eneo la hifadhi ya barabara mnawachukulia hatua za kisheria, maana wanaofanya hivi ni maaudui wa maendeleo kwelikweli”, alisema Pinda.
Pinda aliwataka wananchi wa Manyoni na Singida kwa jumla kutumia rasilimali walizonazo kuhakikisha barabara ya barabara hiyo inawapataia maendeleo wanayotarajia, na kuonya kuwa wasipofanaya hivyo watabaki kuona kuwa inawanufaisha wenye baiskeli na magari tu.
Mapema, mkuu wa mkoa wa Singida, parceko Kone alisema, yeye na viongozi wenzake mkoani watahamasisha wananchi kuitumia barabara hiyo katika kuinua uchumi wa eneo hilo kwa kuifanya chachu ya kukuza biashara baina yao na maeneo ya nye ya mkoa huo.
HABARI KATIKA PICHA
Hivi ndvyo jukwaa kuu llilivyokuwa liamenakishiwa kwa ajili ya uzinduzi wa barabara hiyo.Jiwe lamsingi la izinduziWAZIRI wa Miunfombinu,Dk. Shukuru Kawambwa (kushoto) akiwahoji taarifa mbalimbali watendaji wa TANROADS, kuhusu barabara ya Dodoma-Manyoni, alipoikagua kabla ya kuzinduliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANROADS, Crispian Ako. Kina mama wakicheza ngoma kushangilia uzinduzi huo.NAIBU Waziri wa Miunfombinu Ezekiah Chibulunje akisalimia wananchiWAZIRI wa Miundombinu,Dk. Shukuru Kawambwa akisalimia wananchi wa Manyoni, kabla ya hotuba yake ya kumkaribisha Waziri Mkuu kuzindua barabara hiyo.Dk. Kawambwa, Katibu Mkuu wa wizara ya Miundombinu, Chambo na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, wakifuatilia kwa makini hotuba ya uzinduzi ya Waziri Mkuu.WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda akimtambulisha kwa wananchi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Baraara nchini (TANROADS) Ephraim Mrema, wakati wa uzinduzi wa barabara ya Dodoma-Manyoni uliofanyika mjini Manyini jana.WAZIRI Mkuu akizindua jiwe la msingi la kukamilika kwa barabara hiyoWAZIRI Mkuu Mizengo Pinda na mkewa, Tunu Pinda wakiodoka katika uwanja wa shule ya Tambukareli, wilayani Manyoni baada ya kuzindua barabara ya Dodoma-Manyoni. Kushoto ni Waziri wa Miundombinu, Dk.Shukuru Kawambwa na Mkuu wa mkoa wa Singida, Parseko Kone.WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda akikata utepe kuzindua barabara ya Dodoma-Manyoni, katika sherehe zilizofanyika juzi, mjini Manyoni. Kulia kwake ni Waziri wa Miundombini, Dk. Shukuru Kawambwa na kushoto kwake ni mke wake, Tunu Pinda.Ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 126 uegharimu sh. bilioni 143 WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda na mke wake, Tunu Pinda,wakiagana na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dodoma,Betty Mkwasa baada ya kuzindua barabara hiyo.Betty ni Mkuu wa wilaya ya Bahi mkoani humo. Kina mama wakishangilia baada ya Waziri Mkuu Mizengo Ponda kuzinfua barabara hiyo.WAZIRI Mkuu akiondoka na msafara wake baada ya uzinduzi huo
WANAFUNZI wa shule ya sekondari ya Manyoni wakifutahia barabara hiyo mpya kwa kuendesha baiskeli zao baada ya kuzinduzi huoMOJA ya maeneo yaliyozingatiwa katika ujenzi wa barabara hiyo nikuwekwa njia za wanedesha baiskeli kama hawa waliokuwa wakiendesha baiskeli zao katika barabara hiyo.Moja ya madaraja yaliyopo kwenye barabara hiyo.Barabara ikiwa na moja ya mabango au alama za barabarani ambazo hasipswi kunyofolewa na wezi kama ilivyoelezwa kufanyika katika eneo la ChikuyuPOLISI wa usalama barabarani akiwa amelisimamisha lori katika eneo inakoishia lami ya barabara hiyo ya Dodoma-Manyoni. eneo hilo ni la kilometa 55 kutoka Manyoni hadi Isuna ambalo nalo litakamilika kuwekwa lami mapema mwakahuu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269