Breaking News

Your Ad Spot

Apr 29, 2010

AJALI YA BARABARANI TANGA YAUA WANAFUNZI 18 WA MADRASA, 25 WAJERUHIWA

WANAFUNZI 18 wa Chuo cha Kiislamu cha Shamsil-Maariff cha jijini hapa, wamekufa papo hapo na wengine 125 kujeruhiwa baada ya lori walilokuwa wakisafiria kupinduka.
   Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Adolphina Kapufi, alisema ajali hiyo ilitokea jana saa 5.30 usiku katika eneo la njia panda ya Mabanda ya Papa jijini hapa.
  Waliokufa katika ajali hiyo na kutambuliwa ni Twalib Kunemu, Juma Idd, Faraji Habib, Jahshi Rashid, Hussein Bakari, Hajji Athumani na Yussuph Hussein na kwamba kazi ya kuwatambua inaendelea.
   Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Paschal Kanyinyi, alisema kazi ya kutambua maiti waliokufa katika ajali hiyo inakwenda sambamba na utambuzi wa majina ya majeruhi waliolazwa katika wodi ya Galanosi katika Hospitali ya Mkoa, Bombo.
  Alisema majeruhi 125 walifikishwa hospitalini hapo usiku baada ya ajali hiyo kutokea, ambapo 70 kati yao walipata matibabu na kuruhusiwa kurejea chuoni.
Wengine 55 wanaendelea na matibabu katika hospitali hiyo chini ya usimamizi wa timu maalumu ya madaktari na wauguzi.
    Majeruhi waliotambuliwa ni Jumaa Salim ambaye ameumia mbavu, Makame Ahmed, Ahmed Shehe, Selemani Said na Juma Akida. Hata hivyo, aliwataja majeruhi wengine ambao hali zao ni mbaya na wamepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam Kitengo cha Mifupa (MOI) kuwa Hemed Shaaban na Hassan Adam.
   Mwalimu wa zamu wa chuo hicho, Ustaadh Ajali Ramadhan, alisema wanafunzi hao walikuwa wakitokea kijiji cha Kibafuta ambako walikwenda kuhudhuria sherehe za Maulid.
   Hata hivyo, alishangaa kuona idadi kubwa ya wanafunzi waliopata ajali hiyo, kwani walioruhusiwa kutoka chuoni hapo ni 60 tu.
   Kaimu Mganga huyo alimshukuru Mkurugenzi wa Kampuni ya Raha Leo, Seleman Abdallah kwa kutoa msaada wa dawa kwa ajili ya kuwatibu majeruhi waliopata ajali hiyo.
Askari wa kikosi cha usalama barabarani Wilaya ya Tanga, akichukua taarifa za majeruhi waliopata ajali katika ya gari aina ya Fuso lililokuwa likiwasafirisha wanafunzi wa chuo cha kiislamu cha Shamsil-Maariff cha Duga Jijini Tanga waliokuwa wakitokea kwenye Maulid yaliyofanyika Kijiji cha Kibafuta kilichopo mpakani mwa Wilaya ya Tanga na Mkinga jumla ya umla ya wanafunzi 18 walikufa na wengine 125 walijeruhiwaMadaktari na wauguzi wakiwapatia matibabu majeruhi.Majeruhi Ali Maulid akiwa katika wodi ya Galanosi Hospitali ya Bombo baada ya gari aina ya Fuso lililokuwa likiwasafirisha wanafunzi wa chuo cha kiislamu cha Shamsil-Maariff cha Duga Jijini Tanga waliokuwa wakitokea kwenye Maulid yaliyofanyika Kijiji cha Kibafuta kilichopo mpakani mwa Wilaya ya Tanga na Mkinga jumla ya umla ya wanafunzi 18 walikufa na wengine 125 walijeruhiwa.
Majeruhi aliyetambulika kwa jina moja la Hassan akiwa amekatika mokono amelazwa katika wodi ya Galanosi Hospitali ya Bombo baada ya gari aina ya Fuso lililokuwa likiwasafirisha wanafunzi wa chuo cha kiislamu cha Shamsil-Maariff cha Duga Jijini Tanga waliokuwa wakitokea kwenye Maulid yaliyofanyika Kijiji cha Kibafuta kilichopo mpakani mwa Wilaya ya Tanga na Mkinga jumla ya umla ya wanafunzi 18 walikufa na wengine 125 walijeruhiwa. HABARI NA PICHA ZOTE NA MDAU SOPHIA WAKATI


.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages