Breaking News

Your Ad Spot

Apr 30, 2010

UCHAGUZI MKUU SIMBA WAWA KIMBEMBE

WAMBURA, KADUGUDA, ALMAS NA HANSPOPE WAONDOLEWA KUGOMBEA
KINYANG'ANYIRO cha uchaguzi mkuu wa klabu ya soka ya Simba, kimeendelea kukumbwa na mizengwe baada ya  wagombea wanne kati ya watano walioliokua wemewekewa pingamizi kuenguliwa.
   Kulingana na taarifa ambayo imetolewa na kusainiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Deogratias Lyatto uamuzi huo umefanywa baada ya kuridhika kuwa wagombea hao umewana upungufu ambao unawanyima nafasi ya kuwania uongozi.
   Alisema maamuzi hayo yamefanywa bila ya kuwa na lengo la kumharibia mtu yeyote, ila alisema yamefanywa na kamati yake kwa kuzingatia kanuni na taratibu husika kuhusiana na pingamizi zilizowekwa.
  "Hayo ni maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya TFF, ambayo kulingana na katiba ya shirikisho bado wagombea wanahaki ya kupinga maamuzi hayo kwa Kamati ya Rufaa ya shirikisho hilo endapo kama kuna mgombea hatoridhika na uamuzi uliotolewa," alisema.
  Alisema kikao cha kamati yake kilifanyika kati ya Aprili 26 na 28, mwaka huu ili kuzijadili rufani hizo, ambazo alisema zilikatwa na wanachama wa klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam.
  Lyatto aliwataja wagombea waliongeliwa na nafasi walizokuwa wakiwania katika mabano ni Chano K.H.Almasi(Ujumbe wa Kamati yaUtendaji) na Mwina Kaduguda(Makamu Mwenyekiti), Zacharia Hans Poppe na Michael Wambura(Mwenyekiti).
  Lakini wakati wagombea hao wakikumbwa na panga hilo la kamati ya Uchaguzi ya TFF, lakini nuru ya Ismail Aden Rage ambaye alikuwa ni miongoni mwa wagombea waliokatiwa rufaa imeendelea kung'aa.
  Mgombea huyo ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania(FAT) na sasa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), ameibuka kifua mbele, baada ya rufani iliyokatwa dhidi yake na Nassoro Ally kupinga kuweko kwenye kinyang'anyiro hicho, kutupwa.
   Alisema kamati imepitia rufani ambayo ilikatwa na Ally dhidi ya Rage, kuwa kamati imeridhika kwamba kesi zote ambazo zimsababishia kuhukumiwa kifungo jela zilisafishwa na Mahakama Kuu baada ya mgombea huyo(Rage) kukata rufaa.
  "Kamati baada ya kungalia na kupitia rufani ya mwanachama Ally, iliona mgombea tayari alisafishwa na Mahakama Kuu katika kosa ambalo awali lilimtia hatiani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu," alisema.
   Akifafanua kuhusiana na kuenguliwa kwa Chano, ambaye aliwekewa pingamizi na mwanachama, Asha Kigundula, alisema baada ya kupitia ruafani ya Asha imebaini na imeridhika mgombea Chano, hakutimiza wajibu wake kulingana na katiba ya Simba ibara ya 19 kifungu namba 3,4,6,7 na 8 na ibara ya 21 kifungu (g)  na ( i).
   Alisema aidha kamati imebaini mkanganyiko wa majina ya mwombaji uongozi, akitoa mfano alisema kwenye maelezo binafsi ametumia jina la Karaha Hassani Almasi Chano, wakati kwenye kadi ya uanachama wa Simba SC ametambulika kwa jina la Chano K.H. Almasi.
   Hivyo kwa kutotimiza wajibu wake kulingana na matakwa ya katiba ya Simba na mkanganyiko huo wa majina, hakika umeitia dosari fomu ya mgombea husika na hivyo amekosa sifa ya kuwa mmoja wa wagombea," alisema.
  Akizungumzia kuondolewa kwa Kaduguda, alisema aliwekewa pingamizi na mwanachama, Asha Kigundula na kamati imebaini mgombea huyo hakutimiza wajibu kulingana na katiba ya Simba SC ibara ya 19, kifungu namba 3,4,5,6,7,8 na ibara ya 21 kifungu f,g,h,i na ibara ya 38 kifungu namba 4,5,6 na 7.
  "Baada ya kupitia pingamizi hiyo ya Asha, kamati imeridhika kuwa Kaduguda emeshindwa kukidhi matakwa ya kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF, ibara ya 9. Hivyo kamati imemwondoa mgombea kwenye mchakato," alisema.
  Kufuatia kitendo hicho ambacho kimezua minong'ono kwa baadhi ya walioenguliwa na wanachama, vile vile kumezua tetesi kuwa kuna uwezekano wa wanachama au waliongeliwa kulipeleka suala hilo mahakakamani.
  Lyatto alisema kuenguliwa kwa Hans Poppe, ambaye alikua amewekewa pingamizi na mwanachama, Issa Ruchaki, baada ya kubaini kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF ibara ya 25(2).
  Alisema kamati yake ilibaini kamati ya uchaguzi ya Simba ilifanya makosa kwa kutumia ibara ya 45 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya kuzingatia katiba ya klabu hiyo ibara ya 26(5) kwa kumpitisha mwombaji asiyekidhi matakwa ya kifungu hicho.
  Kuhusiana na kuenguliwa kwa Wambura, alisema mgombea huyo aliwekewa pingamizi na mwanachama, Daniel Kamna na kamati yake ilikubaliana na maamuzi ya yaliyotolewa na Kamati ya Uchaguzi na Rufaa za TFF za mwaka 2008.
  Alisema uamuzi huo ulionyesha kuwa Wambura hakukidhi matakwa ya ibara ya 29(7) ya katiba ya TFF na ibara ya 9 ya kanuni za uchaguzi wa wanachama wa shirikisho hilo wakati alipokua kuwania nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF.
  "Hivyo kulingana na maamuzi yaliyotolewa na kamati hizo za Rufani na Uchaguzi za TFF, kamati yangu imemwondoa mgombea huyo,"alisema.
   Hivyo hofu imeendelea kushamiri kutokana na ukweli kuwa, endapo kama wanachama au mgombea yeyote yule atashindwa kufuata taratibu za kukata rufaa kwa Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) kama inavyotakiwa na taratibu husika za shirikisho hilo.
  Badala yake mwanachama au mgombea akalipeleka suala hilo mbele ya mahakama ili kusaka haki yake, ni wazi kuwa uchaguzi huo huenda ukashindwa kufanyika Mei 9, mwaka huu.
  Hali hiyo inatokana na ukweli kuwa kulingana na katiba ya TFF, Klabu na vyama shirikishi vya shirikisho hilo, hazituhusu masuala ya soka kupelekwa mahakamani.
Wambura acharuka
MGOMBEA nafasi ya Mwenyekiti kwenye uchaguzi mkuu ujao wa klabu ya soka ya Simba, Michael Wambura ambaye ameenguliwa kwenye kinyang'anyiro hicho, ameapa kupigana kufa na kupona ili kutetea haki yake.
   Akizungumza muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka(TFF), Deogratias Lyatto kutangaza matokeo ya pingamizi zilizowekwa kwa wagombea.
    Wambura aliyasema hayo kwenye ukumbi wa shirikisho hilo ulioko uwnaja wa Karume.
Tanzania(TFF), ikiwa ni muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF,
   Wambura alisema kwa sasa anasubiri kupatiwa nakala ya kuenguliwa kwake, ambayo alisema ataipata kutoka kwa kamati ya uchaguzi ya shirikisho.
   "Binafsi sishangazwi na taarifa ambazo zimetolewa leo(jana) na Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya TFF, Lyatto. Kwani kilichokua kikiandikwa na vyombo vya habari ni ndicho hicho kilichotokea," alisema.
   Alisema anawasiliana na wanacheria wake ili kuona kuwa ni jinsi gani atafanya, ili kumwezesha kuitetea haki yake ambayo alisema inaonekana dhahiri kupokwa na baadhi ya watu kwa maslahi yao binafsi.
   Wambura ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania(FAT) na sasa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), alisema tangu mchakato wa upitiaji wa majina ya wagombea ulipoanza katika kamati ya Uchaguzi ya Simba.
  Alisema tayari kuna watu(hakuwataja majina), ambao alisema walikuwa wanafanya mbinu chafu hata kutumia kiasi kubwa cha fedha ili kumchafua na asipate tiketi ya kuingia kwenye uchaguzi huo.
  "Pamoja na kuwa kanuni za uchaguzi zineelekeza tunaweza kukata rufaa kwa Kamati ya Rufaa ya TFF, lakini sitasema hivyo kwanza nasubiri nipate hiyo nakala na kisa nitazungumza na wanasheria wangu," alisema.
  Wambura alisema wanasheria wake ndiyo watakuwa na jukumu la kumweleza kuwa nini anapaswa kukifanya, baada ya kutangazwa kuengeliwa kwenye mchakato huo.
  "Kuna kipengele cha 'Integrity'(kukosa uaminifu) ambacho mara kwa mara wamekuwa wakikitumia juu yangu, lakini nitaka wanielezee zaidi ni kuhusiana na kitu hicho ambacho kinanichafua mara zote," alisema.
  Akijibu swali kama ana mpango wowote ule wa kulipeleka suala hilo mahakamani, alisema ni mapema mno kwake kuzungumzia jambo hilo.
  "Siwezi kuzungumzia suala la kwenda mahakamanin sasa, kwani kulingana na kanuni ya uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) ibara ya 12 inaelekeza mgombea kufuata taratibu na kukata rufani kwa Kamati ya Rufaa, kama ikishindikana baadaye Kamati ya Nidhamu ya shirikisho hilo," alisema.
   Kuenguliwa kwa Wambura, Zacharia Hans Poppe na Hassan Dalali kwenye nafasi hiyo kumeifanya nafasi hiyo isaliwe na wagombea watatu, ambao ni Hassan Othman'Hassanoo' , Andrew Tupa na Ismail Aden Rage.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages