BAADA ya mapumziko ya jana, michuano ya Kili Taifa Cup, itaendelea kesho katika kituo cha Iringa, kwa timu za Pinda Boys ya Rukwa Kinondoni Kombaini, Mapinduzi Stars ya Mbeya na Iringa kushuka dimbani katika mechi mbili tofauti kwenye Uwanja wa Samora mjini hapa.
Mechi iliyopangwa kuanza saa 8 mchana, itazipambanisha Rukwa na Kinondoni katika mpambanao unaotarajiwa kuwa na upinzani mkubwa baada ya timu ya Kindondoni kushindwa kuitambia Iringa katika mechi yao jana kwa kutoka sare ya bao 1-1 na Rukwa nayo ikiwa na maumivu ya kutunguliwa na Mbeya bao 1-0 katika juzi hiyo hiyo.
Katika mechi ya saa 10 jioni, nyasi zinatarajiwa kuumia vilivyo kwa mechi ya Mbeya na Iringa ambao ni wenyeji itakayoonyesha ni nani zaidi kati ya timu hizo kwa kuwa kila moja ina bao moja kibindoni ambalo ilipata katika mechi zake jana ambapo Mbeya ilitungua Rukwa na Iringa nayo kupata sare ya 1-1 na Kinondoni.
Mchuano hiyo ambayo ni katika hatua ya makundi, timu nne zilizopo katika kituo hiki cha Iringa zinapambana ili kupata timu mbili zitakazokwenda mjini Dar es Salaam, kuungana na timu nyingine zitakazopatikana kutoka vituo vingine vitano ambako michuano hiyo inaendelea katika hatua ya makundi ambavyo ni Mwanza, Arusha, Mtwara, Dodoma na Tanga.
Katika michuano hiyo ambayo imedhaminiwa kwa mamilioni ya fedha na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanajaro Premier Lager, mshindi wa kwanza atazizolea zawadi ya sh. milioni 35, wapili sh. milioni 20, watatu milioni tano huku mchezaji bora, kipa bora, mfungaji bora, kocha bora na timu yenye nidhamu wakipata sh. milioni mbili kila mmoja.
mwisho
Your Ad Spot
May 9, 2010
Home
Unlabelled
KILI CUP IRINGA KUELNDELEA KESHO
KILI CUP IRINGA KUELNDELEA KESHO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269