*Ni kutokana na kesi iliyopelekwa na Wambura baada ya kuenguliwa kuwania uenyekiti
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo imesimamisha kwa muda uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba iliokuwa umepanga kufanyika Jumapili, Mei 9, 2010.
Hatua hiyo imefuatia mahakama hiyo kukubali malalamiko ya Michael Wambura aliyekuwa mmoja wa wanachama aliyekuwa anawania kugombea Uenyekiti katika uchaguzi huo lakini akaenguliwa na kamati ya rufani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakati wa mchujo.
Pamoja na Wambura kuiomba mahakama kumsakia haki itendeke aliitaka mahakama hiyo pia imlinde asichukuliwe hatua yoyote kwakufikisha suala hilo mahakamani hadi shauri kuu litakapoamuliwa.Kwa mujibu wa Katiba ya FIFA inayofuatwa pia na CAF, CECAFA na TFF ni marufuku kupeleka swala lolote mahakamani. Shauri kuu la kesi hiyo limepangwa kusikilizwa mei 31, 2010 na hakimu Rita Tarimo.
Hii ndiyo ruling iliyotolewa na hakimu Tarimo leo
Your Ad Spot
May 6, 2010
Home
Unlabelled
MAHAKAMA YASIMAMISHA UCHAGUZI WA SIMBA
MAHAKAMA YASIMAMISHA UCHAGUZI WA SIMBA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269