HATUA YA MAANDALIZI YAIVA KITUO 'E' CHA IRINGA
Story
MICHUNANO ya Kili Taifa Cup katika hatua ya makundi, inaaza kutimua vumbi Jumamosi hii katika vituo vyot sita huku maandalizi hatika kituo ‘E’.cha mkoa wa Iringa akielezwa kukamilika.Msimamizi wa kituo cha Iringa, Eliudi Mvera alisema Pinda Boys kutoka mkoa wa Rukwa na Mapinduzi Stars ya Mbeya ndizo zitafungua dimba kwa kupepetana katika mechi itakayoanza saa 8 mchana na baada ya mechi hiyo timzu ya mkoa wa Kinondoni itajitupa kilingeni na wenyeji katika kituo hicho, Ruaha Stars ya Iringa.
Alisema, timu timu zitakazomenyana katika kituo chake, zilimeshawasili tangu jana.
Kulingana na ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Soka nchini TFF, Jumapili itakuwa mapumziko na Jumatatu ndiyo Mbeya na Iringa zitaanza kuvaana na baadaye siku hiyo kumalizwa kwa kupambana timu za Kinondoni na Rukwa.
Jumanne pia ni mapumziko
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269