Breaking News

Your Ad Spot

May 16, 2010

NAPE ATANGAZA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA UBUNGO




MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Bakhresa, Mazese jijini Dar es Salaam, leo, ambapo alitangaza nia yake ya kuwaniua Ubunge jimbo la Ubungo.
**Mkutano wake wafunika Viwanja vya Manzese-Bakhresa
MJUMBE wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Ubungo katika uchaguzi mkuu utakaofayika Oktoba mwaka huu.
   Nape ambaye pia ni Katibu Msaidizi wa Idara ya Mambo ya Nje ya CCM, alitamgaza nia hiyo leo katika viwanja vya Bakhresa Manzese Dar es Salaam katika  mkutano wa kuwapongeza wana-CCM kwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
   Alisema amefikia uamuzi huo kutokana na kuwa na nia ya dhati ya kuliletea maendeleo jimbo la Ubungo hasa baada ya kuombwa kwa muda mrefu na wakazi wa jimbo hilo.
   "Japo niliombwa muda mrefu kujitokeza kuliongoza jimbo hili, ilinilazimu kuchukua muda mrefu kulifanyia kazi ombi hilo kwa kuwa ubunge si jambo la mchezo kwanini suala linalohusisha kuwaongoza watu na kuwaletea maendeleo, lakini sasa nimekubali kwa kuwa uwezo ninao," alisema Nape.
   Alisema sifa zinazohitajika kuwanazo kiongozi na kuwa mwakilisha wa wananchi anazo ikiwemo kukubalika na wapiga kura, hivyo ameamua kujitosa kuwania akiwa na uhakika wa kufanikiwa.
   Kwa mujibu wa Nape, licha ya miundombinu muhimu kwa wananchi inayosambaza maji na umeme kwa jiji kupita katika jimbo hilo, lakini bado wakazi wake hawajanufaika ipasavyo, hivyo hulo limezidisha haja yake ya kutaka kuwa mwakilishi wake bungeni ili kutetea haki za wakazi.
  Alisema ameweza kujitokeza mbele na kupinga mikataba mibovu iliyoingiwa wakati wa ujenzi wa jengo la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), na kufanikiwa kuokoa zaidi ya sh. bilioni nane, hivyo hatoshindwa kuwawakilisha vyema wananchi wa jimbo la Ubungo.
  Mjumbe huyo wa NEC aliwataka wananchi wa jimbo hilo kuwa makini na baadhi ya watu wanaojipitisha na kutoa posho kwani hizo ni pesa walizozipata kwa njia haramu.
  "Zikija hela za digidigi, tembo na swala nyie zipokeeni kwa vile hawakuzipata kwa njia ya halali, lakini la muhimu ni kuwa makini na kujua mtu mwenye dhamira ya dhati ya maendeleo ya jimbo hili," alisema.
  Katika mkutano huo jumla ya sh. 63450 zilichangwa na wana-CCM kwa ajili ya kumchangia Nape kuchukulia fomu za ubunge endapo atakapopitishwa na Chama kukiwakilisha katika nafasi hiyo.
  Mbali na kiasi hicho, UVCCM kata ya Makubuli katika jimbo hilo nayo ilimchangi sh. lakini moja kwa ajili ya kuchukulia fomu za ubunge.
Nauye akisindikizwa na Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM Kata ya Ubungo, alipowasili kwenye Viwanja wa Bakhresa-Manzese, Dar es salaam, leo kuhutubia mkutano wa hadhara na kutangaza nia hiyo ya kuiwania ubunge.Watu wakimsikiliza Nape

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages