Na Mohammed Mhina na Christina Mponji wa Jeshi la Polisi
Matatizo ya ajali za barabarani yanayosababishwa na uwezo duni wa madereva katika fani hiyo nchini sasa kupatiwa ufumbuzi baada ya kubuniwa kwa mfumo mpya wa utoaji wa leseni kwa madereva.
Akizindua mafunzo ya siku mbili kwa wakuu wa polisi mikoa na mameneja wa TRA mikoa yanayofanyika katika chuo cha usimamizi wa kodi, Inspekta Jenerali wa Polisi Said Mwema amesema mfumo huo wa utoaji wa leseni utazingatia uwezo, ubora na kiwango kizuri alichonacho dereva kabla ya kupatiwa leseni.
“Dereva atapimwa uwezo wake ili kujua kama ana sifa zinazostahili kupata leseni na endapo atabainika kutokuwa na sifa zinazokidhi mahitaji basi dereva huyo hatapewa leseni”, alisema Bw. Said Mwema.
Akizungumzia Lengo la kuanzishwa kwa mpango huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini alisema ni kudhibiti utoaji holela wa leseni jambo linalochangia utoaji wa leseni kwa madereva wasio na viwango vinavyolingana na madaraja ya leseni wanazopewa pamoja na utengenezaji wa leseni feki.
Ameongeza kuwa leseni hizo zitasaidia kudhibiti madereva watakao fanya makosa katika mkoa mmoja na kukimbilia mkoa mwingine ili kupata leseni nyingine baada ya kufungiwa leseni zao kutokana na makosa yao.
Viongozi Wakuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini wameanza kupatiwa mafunzo juu ya mchakato wa utoaji wa leseni mpya za udereva hapa nchini.
Akifungua mafunzo hayo, mkuu wa jeshi la polisi nchini inspekta jenerali Said Mwema, amesema mafunzo hayo ya pamoja ni mchakato wa kuelekea kwenye utoaji wa leseni za kisasa ambao utaanza kutekelezwa kwa awamu kwenye mikoa tisa ya Tanzania bara.
IGP amesema leseni hizo zitasaidia kuwatambua madereva watakaofanya makosa katika mkoa mmoja na kukimbilia mkoa mwingine kupata leseni. Leseni hizo bado gharama zake hazijafahamika na imeelezwa kuwa zina alama nyingi za kiusalama na itatumia mfumo wa TEKNOHAMA ambayo inahifadhi kumbukumbu zote za muhusika zitakazosaidia kumtambua kama amefanya kosa.
Nae Mkurugenzi wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Kamishna Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mohammed Mpinga wameelezea mambo yatakayozingatiwa katika utoaji wa leseni hizo mpya.
Kwa upande wake Kamishna wa idara ya kodi za ndani wa TRA Bw. Patrick Kassera alisema leseni ya kwanza inatarajiwa kutolewa septemba 15, mwaka huu.
Alisema pia utoaji wa leseni hizo utatoa kipaumbele kwa wale wenye leseni za zamani na ambao watafanyiwa majaribio upya ili kuangalia uwezo walionao kabla ya kupatiwa leseni hizo mpya na kuwataka wenye leseni za zamani kuendelea kutumia leseni zao hadi hapo watakapopatiwa leseni mpya.
Utoaji wa leseni mpya utahusisha mikoa tisa katika awamu ya kwanza ambayo ni Tanga, Arusha, Kilimajaro, Mwanza, Mbeya, Dodoma na mikoa mitatu ya kanda maalum ya kipolisi ambayo ni Kinondoni, Temeke, na Ilala
Viongozi wanaoshiriki kwenye mafunzo hayo ni Wakuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini pamoja na Wakuu wa TRA wa mikoa tisa inayolengwa kuanzishwa kwa utuaji wa leseni hizo
Akifungua mafunzo hayo, mkuu wa jeshi la polisi nchini inspekta jenerali Said Mwema, amesema mafunzo hayo ya pamoja ni mchakato wa kuelekea kwenye utoaji wa leseni za kisasa ambao utaanza kutekelezwa kwa awamu kwenye mikoa tisa ya Tanzania bara.
IGP amesema leseni hizo zitasaidia kuwatambua madereva watakaofanya makosa katika mkoa mmoja na kukimbilia mkoa mwingine kupata leseni. Leseni hizo bado gharama zake hazijafahamika na imeelezwa kuwa zina alama nyingi za kiusalama na itatumia mfumo wa TEKNOHAMA ambayo inahifadhi kumbukumbu zote za muhusika zitakazosaidia kumtambua kama amefanya kosa.
Nae Mkurugenzi wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Kamishna Paul Chagonja, Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mohammed Mpinga na Kamishna wa kodi za ndani wa TRA Bw. Patrick Kassera, wameelezea mambo yatakayozingatiwa katika utoaji wa leseni hizo mpya.
Naye Mtaalam mshauri wa Mradi wa Taifa wa Leseni za Udereva nchini Bw. Alnoor Nkya, ameelezea muuondo na sifa za leseni hizo.
Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yanafanyika kwenye Chuo cha Usimamizi wa Kodi Jijini Dar es Salaam, pia yanahudhuriwa na Makamanda wa polisi wa mikoa.
ikoa itakayohusika na mchakato huo wa utoaji wa leseni mpya ni Arusha , Dodoma, Kilimanjaro, Tanga,Mwanza,, Mbeya, na mikoa mitatu ya kanda maalum ambayo ni Ilala, Kindoni, na Temeke ambayo makamanda wake wote wamehudhuria.
Your Ad Spot
Aug 25, 2010
Home
Unlabelled
UTOAJI HOLELA WA LESENI KUDHIBITIWA
UTOAJI HOLELA WA LESENI KUDHIBITIWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269