Breaking News

Your Ad Spot

Sep 9, 2010

MAANDALIZI YA EID EL FITR

MBUZI ni miongoni mwa vitoweo ambavyo hupendwa sana kuliwa nyakati za siku kuu. Pichani, wauzaji wa mifugo hiyo wakisubiri wateja, ambao wangefika kununua mbuzi kwa ajili ya kumla wakati wa sikukuu ya Iddi El Fitr, inayotarajiwa kuwa leo, kufuatia kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.(Picha na Bashir Nkoromo).

MSIMAMIZI wa Masoko wa Zantel mkoa wa Tanga, Humphrey Lyimo, akikabidhi msaada wa vyakula kwa mwenyekiti wa kikiundi cha kina mama wa kiislamu wilaya ya Muheza, Tanga kwa ajili ya kuwalisha yatima na watoto wa mitaani wakati wa sikukuu ya Eid Il Fitr, jana. (Na Mpigapicha Maalum).
Naibu Khadhi Mkuu wa Zanzibar Shekhe Khamis Haji Khamis akiwakabidhi akiwakabidhi Mafuta ya kula watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu wa mjini Unguja Zanzibar mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Vodacom Foundation kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation na kutoa misaada ya vyakula, mafuta ya kula,madafutari pamoja na mbuzi 12 kwa ajili ya sikukuu ya Eid el Fitr,Vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 2.
ASHA suleimani, mkazi wa Kichangani, Tandika, Dar es Salaam, akimsuka nywele mtoto wake, Salma Hassan (6), nyumbani kwao jana, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mtoto huyo kusherehekea sikukuu ya Idd El Fitr inayotarajiwa kuwa leo, kufuatia kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani. (Picha na Bashir Nkoromo).
================================================================
Chachandu Daily inawatakia wadau wote EIF MUBARAK
=======================

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages