Breaking News

Your Ad Spot

Sep 10, 2010

BAADHI YA YALIYOSISIMUA IDD EL FITR LEO

"KIJANA WANGU NAKUTAKIA MAFANIKIO MEMA KATIKA UCHAGUZI MKUU"
RAIS mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, akibusu mkono wa Rais Jakaya Kikwete, kuashiria kutakiana heri ya sikukuu ya Idd el Fitri baada ya sala ya Idd, iliyoswaliwa kitaifa, leo katika Msikiti Mkuu wa Riyadh, mjini Tanga. (Picha na Freddy Maro).
======================================================
"MWAFAKA TAYARI, NAWATAKIENI MAFANIKO MEMA KATIKA UCHAGUZI, ATAKAYESHINDWA AKUBALI"
RAIS wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, akibadilishana mawazo na wagombea urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Sheni (CCM) na Seif Sharif Hamad wa CUF (kulia) baada ya Baraza la Idd el Fitri katika Viwanja vya Jumba la Wananchi Forodhani, Zanzibar, leo. (Picha na Ramadhan Othman).

"SISI SOTE NI KITU KIMOJA TUDUMISHE UPENDO"
MGOMBEA mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Katibu Mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, Forodhani, mjini Zanzibar, jana, ambako walihudhuria Baraza la Idd el Fitri. (Picha na Martin Kabemba).
======================================================
DAR NAKO MAMBO HAYAKUWA MADOGO
MKE wa Rais, Mama Salma Kikwete akisalimiana na waumini baada ya swala ya Idd el Fitr, leo katika msikiti wa Al Farouq, Kinondoni, Dar es Salaam.
SHEIKH wa mkoa wa Dar es Salaam,. Elhad Mussa akitoa hotuba katika sala ya Idd katuika msikiti wa Afarouq, Kinondoni, Dar es Salaa, ambako sala hiyo iliswalimwa kimkoa.
WATOTO kwa wakubwa wakienda kushiriki swala ya Idd el Fitr, leo katika Viwanja vya Ukwamani, Kawe
WAUMINI wakiwa katika msikiti wa Alfarouq, Kinondoni leo.
BAADA ya kuwa na kuku kibindoni sasa, jamaa ananunua viungo. hii ilikuwa leo katika soko la Mwananyamala, Dar es salaam.
USTAADHI akinunua kuku wa kiswahili, katika soko la Mwananyamala kunogesha sikukuu ya Idd el Fitr, kuku huo aliuzwa kwa sh. 7,000 tu.
Kinamama nao wakipigana vikumbo katika duka la viungo vya pilau kwenye soko hilo la Mwananyamala
Mama akijiridhisha kwanza kama kuku huyu ni bomba kwa pilau, kabla ya kumununua katika soko hilo, la Mwananyamala kwa sh. 7,000 tu.
FATUMKA Mussa, mkazi wa msasani, dar es Salaam, akinyonyesha mtoto wake wa kiume aliyemzaa usiku wa kumkia sikukuu ya Idd Etri,  hospitali ya mwananyamala, Dar es salaam. Jumla ya watoto 20 walizaliwa usiku huo katika hospitali ya Mwananyamala, Dar es salaam.(Picha na Bashir Nkoromo).
REHEMA Mtimbwa , mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam, akiwa na watoto wake mapacha wa kike na kiume, aliojifungua usiku wa kuamkia sikukuu ya Idd el Fitri katika Hospitali ya Mwananyamala. Jumla ya watoto 20 walizaliwa. (Picha na Bashir Nkoromo).
SIJUI NINAZO? inaelekea ndivyo alivyokuwa akijiuliza muumini huyu wa kislam, wakati akipekua mfuko wa kaanzu yake ili kupata fedha walau kidogo ya kutoa sadaka iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na muumini mwenzake aliyekinga kapu, kabla ya kuanza ibadaya Idd el Fitr, leo kwenye Viwanja vya Ukwamani, Kawe, Dar es Salaam.
Hakuna kucheza mbali wakati jungu la pilau lipo jikoni. Hapa ilikuwa ni kwenye nyumba moja, Kawe, Dar es salaam.

2 comments:

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages