Breaking News

Your Ad Spot

Apr 13, 2011

HALI YA UCHUMI YATARAJIWA KUWA SHWARI?

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
HALI YA UCHUMI YATARAJIWA KUWA SHWARI
Hali ya uchumi wa dunia inaendelea kuimarika na kuanza kurudi katika hali yake ya kawaida japokuwa bado uwiano halisi haujapatikana. Hayo yamesemwa na Mchumi Mshauri na Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti katika Shirika la Fedha la Kimataifa Bw. Olivier Blanchard.
Akiongea na waandishi wa habari mjini Washington DC. Bw. Blanchard alisema kuwa uchumi wa dunia umeanza kuimarika lakini bado hauja kaa sawa, na hii nitaielezea vizuri katika dakika chache zijazo. Njia nzuri ya kufafanua pointi hii ni kuwapa namba tatu. Kwa uchumi wa Dunia, miaka hii 2011 na 2012 tunategemea uchumi kukua kwa kiwango cha asilimia 4.5 kiwango ambacho ni cha juu na cha kuridhisha, lakini tukiangalia kwa undani zaidi, tutagundua kuwa , kwa uchumi ulioendelea tunatabiria  kuwa asilimia 2.5 tu kwa kila mwaka, na kwa nchi za kipato cha kati na zinazoendelea tunatabiria kuwa asilimia 6.5 kwa kila miaka miwili ijayo, kwahiyo  itakuwa makundi matatu ambayo ni 4.5, 2.5,6.5.
“ Ngoja nianze na habari njema ya juu ya kuimarika kwa uchumi na kurudi katika hali yake ya awali. Awali kulikuwa na woga  kuhusu hali hii ya kudidimia kwa uchumi.Hatukuwashirikisha  kwa hili lakini hali hiyo ilikuwepo. Wasiwasi wetu ulikuwa hasa kwa nchi zile zenye uchumi ulioendelea, lakini tunashukuru kwa sasa hali imekuwa shari na kurudia katika hali yake ya awali. Akiba ya imeongezeka zaidi. Kiwango cha fedha kimeongezeka, sekta binafsi zimekuwa, matumizi yameongezeka na uwekezaji umekuwa.Hii ni habari nzuri sana. Hiki ni kitu ambacho hakija wahi kutokea”. Alifafanua Bw. Blanchard.
Akiendelea kutoa ufafanuzi Bw. Blanchard alisema wasiwasi umekuwa katika bei ya vitu. Bei ya vitu imepanda zaidi ya ilivyotegemewa, inaonyesha ni kiasi gani mahitaji yanazidi uzalishaji. Ongezeko hili linatukumbusha miaka ya 1970 ambapo hali hii ilijitokeza. Hatutarajii kwamba ongezeko hili litaathiri kukua kwa uchumi na kusababisha kurudi nyuma.Alisisitiza Blanchard..
Ukiangalia kwa nchi zilizo na kipato  cha juu, upungufu wa mgawanyo wa mafuta, kupotea kwa malipo na matokeo ya kuporomoka kwa uchumi ukizichanganya taarifa hizi kwa pamoja utagundua kuna madhara lakini sio makubwa sana. Ili kuweza kupanua masoko ya nchi kuna changamoto kubwa na inabidi ziangaliwe kwa mapana zaidi kwa sababu ukiangalia hifadhi iliyopo na mahitaji yanayohitajika ni makubwa na upatikanaji katika masoko yanayochipukia  katika benki kuu ni hafifu. Hivyo kwa nchi zenye masoko yanayochipukia wanatakiwa wawe makini sana, bila kufanya hivyo kuna uwezekano wa uchumi kuporomoka kwa wakati mmoja, lakini inavyoelekea hatutarajii kuathirika kwa kwa ukuaji wa uchumi. Na lengo letu ni kufikia asilimia 6.5, Bw. Blanchard.
Katika kukamilisha taarifa hizi Bw. Blanchard alisema kuwa kuna taarifa ambazo sio nzuri kuhusiana na hali ya uchumi. Kwan nchi karibia zote ambazo zimeendelea wanakumbana na tatizo la upatikanaji wa ajira, mahitaji kuzidi kipato wananchi walichonacho na kwa upande wa mabenki riba ni kubwa na mitaji ni midogo ukilinganisha na mikopo inayotolewa.
Kwa upande wa nchi zinazochipukia katika masoko na kwa upande wao katika sekta ya fedha wanaweza kukabiliana na mtikisiko wa uchumi kwani riba katika mabenki yao ni ndogo sana ukilinganisha na nchi zilizoendelea.
Kwa ujumla agenda za hali ya uchumi duniani inabaki kuwa palepale lakini kwa kipindi maalumu na kwa haraka zaidi. Ili uchumi uimarike, nchi zilizoendelea na zinazochipukia katika masoko lazima zifikie malengo waliyojiwekea na kuunda kwa uangalifu sera za uchumi katika ngazi za kitaifa.
Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji Mkuu - Wizara ya Fedha
Washington DC
11 Aprili, 2011

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages