Breaking News

Your Ad Spot

May 10, 2011

NAPE ATAMBA KUMUUMBUA DK. SLAA KESHO SINGIDA

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema leo atamwaga hadharani jinsi Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbrod Slaa anavyofanya ufisadi wa kutisha ndani ya chama hicho.
Nape alisema ataeleza ufusadi huo, katika mkutano wa hadhara utakaofanyika kwenye Stendi Kuu ya Mabasi mjini Singida mjini, ukiwa ni mkutano wa pili, katika ziara ya viongozi wa Sektretarieti ya Halimashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM waliyoianza jana mkoani hapa.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya jengo la Ushirika Ikungi nje ya mji wa Singida, Nape alisema, anazo nyaraka zinazoonyesha Dk. Slaa na baadhi ya viongozi wa Chadema wanavyojinufaaisha na fedha za chama hicho huku wanachama wenyewe wakiendelea kumpigia makofi.
Katika ziara hiyo ya kujitambulisha msafara wa Sekretarieti hiyo ya CCM, unaoongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Kapteni Mstaafu, John Chiligati Nape amefuatana pia na Katibu wa Uchumi na Fedha, Mchumi Mwigulu Nchemba na Katibu wa Oganaizesheni Asha Juma Abdallah.
Katika mikutano iliyofanyika jana, Ikungi na Ligwa, Nape alikanusha vikali kuwepo wa waraka wa siri wa Sekretarieti mpya ya  CCM ambao Dk. Slaa anadai kuwa nao.
Amesema, kwa kujitapa kwenye majukwaa juzi mjini Sumbawanga, kwamba anazo nyaraka za siri za Sekretarieti hiyo, kwanza inadhimhirisha kwamba hajui nini maana ya siri  na dhahiri.
Nape alisema, anachokiita Dk. Slaa kuwa siri ni udhanifu wa kupuuzwa kwa sababu yote yaliyoainishwa kwa ajili ya kutekelezwa na sekretarieti ya CCM baada ya kikao cha mjini Dodoma, hakuna hata moja ambalo ni siri hadi sasa.
Alisema, baada tu ya sekretarieti kukabidhiwa mikoba, imefanya mikutano ya hadhara zaidi ya kumi katika mikoa mbalimbali na kuelezwa kwa kinaga ubaga nini hasa kilichotokea Dodoma hadi kupatikana kwa sekretarieti mpya.
Nape alisema, pamoja na mambo kadhaa wamekuwa wakieleza wazi kwamba kilichofanyika ni CCM kujifanyia tathmini kuona kama kweli hali ilimo sasa na inatosha kuipigisha hatua ya kuongoza sasa na baadaye.
Alisema, baada ya tathmini hiyo, kama chama komavu kiliyakubali mapungufu kiliyobaini na kuamua kwamba ili kuondokana na mapungufu yaliyobainika, lazima uongozi wa juu uliopo uwajibike, jambo ambalo hakuna chama kingine kinachoeweza kuthubu kikabaki salama.
"Jamani tilichofanya Dodoma ni kuwasha Mwenge kwa ajili ya kuongeza matumaini pale yalipoanza kufifia, kuongeza imani kwa chama pale ilipoanza kudorora, jambo ambalo kwa chama chenye umri mkubwa kama CCM lilikuwa la lazima", alisema Nape.
Akifafanua zaidi kuhusu suala hilo, Chiligati alisema, anachodai kuwa nacho Dk. Slaa na kukiona kuwa ni waraka wa siri, kama kweli anacho ni gamba ililotupa CCM ambalo linamyima usingizi.
Chiligati alisema, kwa kawaida kitu kinapokuwepo muda mrefu sana kisipojitazama upya kuendelea kuwepo kuwa kwa mashaka makubwa, na ndiyo maana CCM imeona umuhimu wa kujitathmini na kuamua bila kusita kujivua gamba.
Alifafanua kwamba, gamba ililojivua CCM si ngozi ila ni yale matendo maovu ambayo baadhi ya viongozi walianza kuyakumbatia kama ufisadi, na kutokifanyaa chama kuwa cha wanachama badala yake kuonekana cha wenye fedha.
Chiligati alisema, kimsingi ufisadi na hali hiyo ya kutokifanya chama kuwa cha wanachama ndilo gamba lililovuliwa toka CCM amabalo sasa Dk. Slaa anataka kutamaba nalo wakati CCM walishaachana nalo tangu mkutano ule mzito wa Dodoma.
Kwa upande wake, Nchemba alisema, kwa kujivua gamba sasa CCM ni mpya, wale waliokuwa wamekimbia kutokana na kero za baadhi ya viongozi, sasa warejee kwa sababu yale hayawezi kujirudia tena.
Alisema, sasa CCM ni  itaendesha mambo yake kisasa na kisayansi zaidi kuliko ubabaishaji, amkbapo mali na miradi ya chama popote ilipo haitaweza kutafunwa na mbadhirifu yeyote bali rasilimali hizo zitakuwa kwa manufaa ya wanachama wote.
Miongoni mwa viongozi wa Sekretarieti hiyo mpya ambao hawapo kwenye ziara hiyo mkoani Singida ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama ambaye ana majukumu mengine.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages