KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Nontsikelelo Sisulu, aliyekuwa mke wa mpigania uhuru wa Afrika Kusini, marehemu Walter Sisulu,katika Ubalozi wa Afrika Kusini mjini Dar es Salaam, leo
Akuzungumza baada ya kutia saini kitabu cha maombolezo ya kifo hicho,
kwenye Ubalozi wa Afrika Kusini mjini Dar es Salaam, Katibu wa NEC,
Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema, CCM imeguswa na kifo hicho kwa
sababu mbali na kuwa mke wa mpigania uhuru, Mama Sisulu alikuwa mstari
wa mbele kupigania haki na usawa wa binadamu.
Nape alisema, katika uhai wake, Mama Sisulu alitumia taaluma yake ya
uuguzi kuwafundisha wauguzi wenzake ambao walihudumua wanaharakati
waliokuwa katika mapambano ya kusaka uhuru wa Afrika Kusini.
Alisema, Mama sisulu atabaki kuwa mfano wa wapenda usawa wa binadamu
duniani kwa sababu hata baada ya Afrika Kusini kupata uhuru, alikuwa
miongoni mwa viongozi waliosimamia maridhiano ya kusahau madhila
yaliyofanywa baina ya makaburu na raia wa Afrika kusini kabla ya uhuru.
Nape alisema, licha ya ukatili na ubaguzi wa rangi waliokuwa wakiufanya
makaburu, lakini maelewano yaliyofanyika baada ya uhuru wa chini ya
wanaharakati akiwemo Mama Sisulu wazungu hawakubaguliwa.
Alisema matendo ya Mama Sisulu yatabakia kuwa mfano bora kwa wapinga
ubaguzi na wapenda amani duniani ikiwemo Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269