Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakiongozwa na Mkurugenzi wa Miradi Maalum, Phocus Lasway (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Fedha, Kelvin wakifanya usafi Barabara ya Uhuru karibu na Soko la Ilala Mchikichini, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, ikiwa ni moja ya shamrashamra ya kuadhimisha Wiki ya Mazingira Duniani iliyofikia kilele Julai 6, mwaka huu. TBL siku hiyo pia ilikabidhi kwa Manispaa ya Ilala,msaada wa vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. mil 11.
Meneja wa Miradi Maalum wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Leonidas Gama, moja kati ya vifaa vya usafi vyenye thamani ya sh. milioni 11 kwa ajili ya Manispaa ya Ilala. Kabla ya kukabidhi vifaa hivyo mwishoni mwa wiki, wafanyakazi wa kampuni hiyo walifanya usafi wa mazingira katika Barabara ya Uhuru, Dar es Salaam,ikiwa ni moja ya shamrashamra ya kuadhimisha Wiki ya Mazingira Duniani iliyofikia kilele Julai 6, mwaka huu
Wafanyakazi wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifanya usafi Barabara ya Uhuru karibu na Soko la Ilala Mchikichini, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, ikiwa ni moja ya shamrashamra ya kuadhimisha Wiki ya Mazingira Duniani iliyofikia kilele jana. TBL siku hiyo pia ilikabidhi
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269