Na Ismail Ngayonga MAELEZO
SERIKALI ya Marekani imeahidi kuipatia Tanzania kiasi cha Dola Milioni 24 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake hapa nchini.
Hayo yamebainishwa na leo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi. Hillary Clinton (pichani) alipotembelea Kituo cha Afya cha Buguruni Jijini Dar-Es-Salaam na kujionea hali ya utoaji wa huduma ya afya.
Alisema kuwa msaada huo wa Serikali yake umetokana na jitihada zilizofikiwa na Serikali ya Tanzania katika kuzuia ukatili wa kijinsia hususani kwa wanawake ambao kwa sasa umeshika kasi katika maeneo mbalimbali duniani hususani katika nchi zinazoendela.
Akifafanua zaidi Waziri huyo alisema ukatili wa kijinsia hususani kwa wanawake una madhara makubwa kiakili na kimwili ikiwemo matukio ya kubakwa, kupigwa pamoja na kumwinya nafasi ya ushiriki wao katika masuala mbalimbali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Alisema mwaka jana (2010) Serikali Marekani ilitenga kiasi cha Dola Millioni 60 kwa ajili ya mirad kuzuiaji wa ukatili wa kijinsia kwa wanawake katika mataifa 39 yanayoendelea duniani, hivyo sasa ni zamu ya Tanzania kuongeza kasi ya mapambano hayo chini ya mradi huo utaotekelezwa katika kipindi cha miaka 3.
“Nimefurahishwa sana nilipofikika kituoni hapa na kuona Baba akimsindikiza mkewe katika kituo cha afya, na hii ni faraja kubwa sana kwani ni jambo geni kabisa kuliona likifanyika katika maeneo mengine hususani katika nchi zinazoendelea” alisema Waziri huyo.
Aidha kwa upande mwingine Waziri huyo amevutiwa na utoaji wa huduma za afya katika kituo hicho ambacho hupokea wagonjwa 5000 kwa siku wanaofika kituoni hapo kwa ajili ya vipimo na matibabu mbalimbali ikiwemo kupima ugonjwa wa malaria, pamoja na kuendesha huduma za uzazi kwa akina mama wajazito na watoto wachanga.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Kituo hicho Dkt. Mwajuma Mbaga alisema wamefurahishwa na ujio wa Kiongozi huyo wa juu katika Serikali ya Marekani ambaye kwa kiasi kikubwa ameonyesha kuguswa kwake na changamoto zilizopo katikakituo hicho na hivyo kutoa ahadi za kupata ufumbuzi wake.
Aidha Dkt Mbaga alisema wamepata faraja kubwa kutembelewa na Waziri huyo katika Serikali ya Marekani ambaye naye binafsi ameonyesha kuguswa na changamoto zilizopo katika kituo hicho na kuahidi kuzipata ufumbuzi wa haraka ili kusaidia wananchi wa Watanzania.
‘Ujio wa Kiongozi huyu wa juu katika Serikali ya Marekani utaongeza na kuimarisha ushirikiano uliopo kati yake na Tanzania ukizingatia kuwa ametembelea wodi mbalimbali na kujionea changamoto zilizopo nayeye binafsi katika hotuba yake ameahidi kutusaidia” alisema Dkt Mbaga
Kuhusu unyanyasaji wa kijinsia hususani kwa wanawake Dkt. Mbaga alisema matukio ya ukatili wa kijinsia ni mengi na yanaendelea kijitokeza katika jamii lakini ni watu wachache wanaojitokeza na kuyaripoti katika mamlaka zinazohusika ikiwemo vituo vya polisi pamoja na hospitlini.
Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa Marekani ambaye ni pia Mke wa Rais wa Zamani wa Marekani Bill Clnton, leo (kesho) anatajia kumaliza ziara yake yake ya Kiserikali nchini ambapo anatajia kukutana na Rais Jakaya Kikwete Ikulu Jijini Dar-Es-Salaam.
Your Ad Spot
Jun 12, 2011
Home
Unlabelled
MAREKANI YAHAIDI DOLA MILLIONI 24 KWA TANZANIA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA
MAREKANI YAHAIDI DOLA MILLIONI 24 KWA TANZANIA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269