Mratibu Mkazi wa Umoja Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou (katikati) akiwasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere kumpokea Naibu Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rose Migiro aliyemaliza muda wake leo wakati
akirejea nchini Tanzania. Kushoto ni Afisa wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa
nchini Hoyce Temu.
Baadhi ya Mabalozi, Wahadhiri na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
wakiwa wamejipanga kumpokea Dr. Asha Rose Migiro.
Msafara wa Dr. Asha Rose Migiro ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za
Nje Mh. Benard Membe (gari la pili) kuelekea sehemu maalum ya mapokezi.
Dr. Asha Rose Migiro akishuka kwenye gari yake baada ya kukanyaga ardhi ya
Tanzania.
Dr. Asha Rose Migiro akipokelewa kwa shangwe na zawadi za maua kutoka kwa
ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje waliofika kumlaki.
Dr. Asha Rose Migiro akisalimiana na baadhi ya mabalozi wapya walioteuliwa na
Mh. Rais hivi karibuni. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini
Dr. Alberic Kacou.
Dr. Asha Rose Migiro akiendelea kusalimiana na Baadhi ya Mabalozi. Kushoto ni
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe
sambamba na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou.
Waziri Membe na Dr. Migiro wakielekea kwenye chumba maalum cha mapumziko
kabla ya mkutano na waandishi wa habari.
Dr. Asha Rose Migiro (katikati), akizungumza na waandishi wa habari nchini Tanzania
baada ya kumaliza muda wake kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
ambapo pamoja na mambo Mengi amesisitiza kwamba hatojihusisha na siasa kwa
sasa. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard
Membe na Kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberic Kacou.
Dr. Asha Rose Migiro akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari
baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere.
Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe.
Dr. Asha Rose Migiro (katikati) akiteta jambo Waziri Membe sambamba na
Viongozi mbalimbali wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini wakiongozwa na
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dr. Alberi Kacou (kushoto) waliofika
kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa JuliusNyerere.
Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji akimpongeza
Dr. Asha Rose Migiro kwa kazi nzuri alipokuwa akitumikia
kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa walipokutana
leo katika Uwanja wa ndege.
Pichani Juu na Chini ni wakinamama wakimwimbia Happy Birthday
Dr. Asha Rose Migiro ikiwa ni maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa
aliporejea nyumbani leo.
Dk. Adha Rose Migiro akisalimiana na wananchi
Kikundi cha Ngoma kikitoa burudani kwa Dr. Migiro (hayupo pichani)
Dr. Asha Rose Migiro akizungumza Jambo na Dr. Alberic Kacou wakati wakitizama
burudani ya ngoma iliyoandaliwa maalum kwa ajili yake. Kushoto ni Waziri Membe.
Dr. Migiro akiwasalimia wasanii wa kikundi cha ngoma.
"Karibu tena Nyumba Mama"... Waziri Membe akiagana na Dr. Asha Rose Migiro baada ya mapokezi.
Dr. Asha Rose Migiro akiagana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dr. Alberic Kacou.
Dr. Asha Rose Migiro akiondoka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere sambamba na ulinzi mkali wakiwemo maafisa wa kimataifa kutoka Ufilipino waliohakikisha ametua nchini Salama. Akizungumza kwenye Iwanja wa Ndege, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) ambaye amemaliza muda wake, Dk. Asha Rose Migiro, amerejea nyumbani leo na kusema kwamba anatarajia kurudi kufundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alikuwa akifundisha kabla ya kuingia kwenye ulingo wa siasa.
Kinyume na matarijio ya watu wengi, Dk. Migiro amesema kuwa kwa sasa hatarajii kujishughulisha katika mambo ya siasa na wala hana mipango ya kugombea urais siku za mbele.
Amesema kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amamteua kuwa Balozi Maalum wa Malaria katika Bara la Afrika na kuongeza kuwa pamoja na kwamba shughuli hizo atakuwa anazifanya kwa muda wake mchache, bado kuna uwezekano mkubwa zikambana na kushindwa kujishughilisha na mambo ya kisiasa. SOURCE MO BLOG
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269