Mkutano wa wazi kwa watu wote kuelimisha umma kuhusu wajibu wa wanaume katika kuzuia maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto utafanyika jijini Dar es salam wiki hii.
taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Ananilea Nkya, imesema mkutano huo utafanyika katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) vilivyoko Mabibo Dar es Salaam Jumatano tarehe 18 Julai, 2012 kuanzia saa 9 hadi saa 11 jioni.
Imesema taarifa hiyo kwamba mkutano huo umeandaliwa na TGNP kwa kushirikiana na shirika linalohamasisha wanaume kushiriki kikamilifu katika mabadiliko ya jamii linalojulikana kama MenEngage.
Dkt. Katanta Simwanza wa shirika la CHAMPION linalojishughulisha na harakati za kuzuia maambukizi ya VVU katika nchi za Afrika ndiye atakayetoa mada kuu kuhusu nafasi ya wanaume kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Watoto wachanga kupata VVU wakiwa tumboni mwa mama yao, wakati mama anapojifungua na kutokana na kunyonya maziwa ya mama yao ni miongoni mwa namna virusi vya ukimwi vinavyoenea barani Afrika.
Mkutano huo lengo lake ni kuuelimisha umma ni mambo gani wanaume wanaweza kufanya ili kuepusha mama mjamzito mwenye VVU kuambukiza mtoto wake anayezaliwa.
Wataalamu wa afya wanasema wanawake wajawazito walioambukizwa VVU wanahitaji matibabu maalumu na uangalizi ili kuepusha wasiambukize watoto wao wanaozaliwa.
Utafiti uliofanywa na mpango wa Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (NACP) mwaka 2009 unaonyesha kuwa watoto 120 hapa nchini wanaambukizwa VVU kila siku.
Aidha utafiti huo pia umeonyesha kuwa kiwango cha maambukizi ya VVU kwa wanawake wajawazito hapa nchini kimefikia asilimia 8.2.
Your Ad Spot
Jul 15, 2012
Home
Unlabelled
MJADALA KUHUSU WANAUME KUZUIA VVU KWA WATOTO KUFANYIKA DAR
MJADALA KUHUSU WANAUME KUZUIA VVU KWA WATOTO KUFANYIKA DAR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269