Breaking News

Your Ad Spot

Jul 12, 2012

MSONDO NA SIKINDE KUONYESHANA KAZI DODOMA KESHO

Bendi kongwe nchini Msondo Ngoma Music na Mlimani Park Orchestra “Sikinde Ngoma ya Ukae” zinatapambana kesho Ijumaa kuanzia saa moja usiku  kwenye ukumbi wa Klab Lazizi Dodoma.
Pambano hilo ambalo tayari limevuta hisia za mashabiki wa muziki wa dansi nchini ikiwemo wabunge   imeandaliwa kwa ajili ya kujua nani zaidi baada ya mwaka jana kuwa na utata wa nani zaidi ambapo kila mmoja alikua anadai yeye ni zaidi.
Akizungumza na waandishi wa Habari Msemaji wa Bendi Ya Msondo ngoma Rajabu Mhamila Super D' alisema
Onyesho hilo pia ni maalum kwa ajili ya kuwaaga mashabiki wao kwa kuwa tunaelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wapenzi wa muziki watajumuika kwa pamoja kwenye Ukumbi huo  hivyo kufurahia
Bendi hizo ambazo zina mashabiki wengi nchini kuliko bendi nyingine zozote, zimeahidi kutowaangusha mashabiki wao kwa kila moja ikijinasimu kuwa itaibuka na ushindi.
Mara nyingi bendi hizo zikipambana huwa ni patashika nguo kuchanika, kwani mbali na mashabiki kushangilia bendi wanazozipenda vibweka na vituko kemkem vimekuwa vikitawala.
Sikinde ambayo iliweka kambi jijini Dar es Salaam imejinasibu kuibwaga Msondo na kudai kuwa hivi sasa haitishi kama ile ya miaka kadhaa iliyopita.
Itakuwa ni mara nyingine tena  kupambana 
 katika pambano hilo mbali na kuwakumbuka wanamuziki wao waliofariki, lakini pia itakuwa ni kusherehekea miaka 50 ya Uhuru huku zikiwa bado zinadumu kwani bendi nyingi za rika lao zimeshafutika kwenye ramani ya muziki nchini.
Sikinde  inayongozwa na Habibu Jeff  uku Msondo ikiongozwa na Mkongwe wa  muziki nchini Muidini Gulumo.
Tunataka mashabiki wa bendi zote wajitokeze kwa wingi bila ya kuwa na wasiwasi kwani watapata burudani ya kutosha , kwani watapiga zile nyimbo za zamani wakati bendi hiyo inaanzishwa mwaka 1978 kama vile 'Selina', Wiki endi', 'Penzi la Fukara', 'Hiba', 'MV Mapenzi namba 1 na 2 hadi za kisasa kama vile 'Supu Umelitia Nazi' na 'Jinamizi la Talaka'.
Naye kiongozi wa Msondo Said Mabera maarufu kama Doctor amesema kuwa kama kawaida yao Msondo ni bendi isiyoshindwa daima.
Mabera amesema kuwa siri ya bendi hiyo kupata ushindi miaka yote ni ushirikiano wanaoupata wanamuziki na wapenzi wao.
Wamewataka wapenzi wao kama kawaida yao kujitokeza kwa wingi na kuishangilia kwa nguvu Msondo Ngoma kwani itaporomosha vibao vya enzi za Nuta, Juwata, Ottu hadi Msondo Ngoma.
Baadhi ya nyimbo zao ni 'Nimuokoe nani', 'Zarina', 'Mwanaidi', 'Kanjelenjele', 'Bahati', 'Sesilia', 'Usiue Usiibe', 'Asha Mwana Seif', 'Kauka Nikuvae', Chuma Chikoli Moto', 'Kilio cha Mzima', 'Ajali', 'Suluhu' na nyingine nyingi.
Kikosi cha Sikinde kitakuwa na Hassan Rehani Bitchuka, Hassan Kunyata, Kaingilila Maufi, Tonny Karama, Shaaban Mabuyu, Habib Abassi, Juma Choka, Ally Jamwaka, Athumani Kambi, Mbaraka Othman, Milambo, Shaaban Lendi, Joseph Benard na Ramadhani Mapesa.

Msondo itawategemea akina Shaaban Dede alijiunga hivi karibuni kutoka Sikinde, Mabera, Abdul Ridhiwani Pangamawe, Saad Ally 'Mashine', Eddo Sanga, Huruka Uvuruge, Zahor Bangwe, Ibrahim Kandaya, Ismail Mapanga, James Mawilla, Muhidini Gurumo, Eddo Sanga, Juma Katundu, Hamisi Mnyupe, Roma Mng’ande `Romario’ na Hassan Moshi.

Aidha Super 'D' alimariza kwa kutaja  ratiba yao ya wiki hii kuwa jumamosi watakuwa Kibaha Kontena kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wake na watamaliza wikiendi katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Dar es salaam siku ya jumapili hivyo wapenzi wajitokeze kwa wingi ili wapate burudani

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages