TANGA, TANZANIA
Wakati siku zikikaribia za kufanyika zoezi la Sensa ya watu na makazi, Mratibu mmoja wa Elimu Kata ya Vugiri wilayani Korogwe, Tanga, Juma Salehe (52) amekamatwa na polisi akihamasisha mitaani kwa kipaza sauti wananchi walikatae zoezi hilo.
Habari zilizofikia meza ya Daily Nkoromo Blog, zimesema mratibu huyo wa elimu ambaye anadaiwa kuwa pia ni Sheikhe wa Msikiti wa Mazinde katika kata hiyo ya Vugiri anashikiliwa katika kituo cha mamlaka mji mdogo wa Mombo uliopo wilani ya Korogwe vijijini mkaoni Tanga.
Imeelezwa amekamatwa jana saa 8.00 mchana ndani ya msikiti wa Mazinde, kutokana na wananchi kutoa taarifa dhidi ya mtu huyo kuendesha vitendo ambavyo vilikuwa vikiwachanganya wananchi kuhusu zoezi hilo la Sensa.
"Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika kwa maandalizi ya shitaka lake", amesema Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga,Coastantin Massawe.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269