BAADHI ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wanawake (UWT) wilaya ya Korogwe Vijijini wakiwa kwenye semina ya ujasiriamali wa kilimo cha alizeti iliyoandaliwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wilayani humo, Dk. Edmund Mndolwa, katika moja ya mikakati ya utekelezaji wa mpango wa kilimo kwanza ili kuwakomboa wananchi hao kiuchumi .
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, wilaya ya Korogwe Vijijini, Dk. Edmund Mndolwa akitoa semina ya ujasiriamali wa kilimo cha alizeti kwa Wajumbe wa Baraza Kuu la Wanawake (UWT) wilayani humo hivi karibuni.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wilaya ya Korogwe Vijijini, Dk. Edmund Mndolwa akizungumza na wananchi wa kata za Bungu, Lulindi na Dundila katika harakati za kuhamasisha kilimo cha alizeti wilayani humo. Kulia ni Katibu wa UWT wilayani humo, Sophia Kupe na Mwenyekiti wa CCM kata ya Bungu, Rashid Mavua.Kushoto ni Diwani wa kata ya Kwadelo, Kondoa, Omari Kariati.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, wilaya ya Korogwe Vijijini, Dk. Edmund Mndolwa akimtambulisha Diwani wa kata ya Kwadelo, Kondoa, Alhaji Omari Kariati kwa wananchi waliohudhuria kupata elimu ya kilimo cha alizeti. Mkutano huo ulifanyika katika kata ya Bungu wilayani humo na diwani huyo alishiriki katika kutoa ushuhuda wa namna kilimo hicho kinavyoweza kuwanufaisha wananchi wa wilaya hiyo kutokana na kata yake kunufaika nacho.
BAADHI ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kuwahamasishwa kulima alizetil katika ya kata ya Magoma wilaya ya Korogwe Vijijini, wakinyoosha mikono kukubali kwamba watalima zao hilo baada ya kupata elimu ya zao hilo. Mkutano huo uliitishwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wilayani humo, Dk. Edmund Mndolwa ambaye amejitolea kuhamasisha wananchi kulima alizeti ili waweze kuondokana na umasikini.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wilaya ya Korogwe Vijijini, Edmund Mndolwa akipata soda na mihogo baada ya kuzungumza na wananchi wa Kata ya Magoma wilayani humo kuwahamasisha kulima alizeti.Kulia ni Diwani wa Kaya hiyo, Khadija Mshahara na kushoto ni Diwani wa kata ya Kwadelo, wilaya ya Kondoa, mkaoni Dodoma.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wilaya ya Korogwe Vijijini, Dk Edmund Mndolwa akiwa pamoja na Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa, Alhaji Omari Kariati wakati wakikagua moja ya shamba la alizeti katika kata ya Mnyuzi wilayani humo.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wilaya ya Korogwe Vijijini, Dk. Edmund Mndolwa akicheza pamaoja na kikundi cha kina mama katika kijiji cha Hale, kata ya Mnyuzi walipomlaki wakati wa kufika eneo la mkutano uliofanyika katika soko kuu la kijiji hicho.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269