Na Elizabeth John
WAKATI singo yake ya ‘Jambo Jambo’ ‘ikiendelea kufanya vema katika
chati mbalimbali za muziki nchini, mkali wa muziki wa bongo fleva, ‘Steve RnB’
ameachia singo mpya inayokwenda kwa jina la ‘Music’, ambayo pia imeanza kutamba
katika tasnia hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, mkali huyo alisema ameamua
kutoa singo hiyo mpya ili kuendelea kuwapa raha mashabiki wake ambao wamekuwa
wakimuunga mkono.
Alisema anayo matumaini makubwa ya wimbo huo kufanya vema katika
medani ya muziki wa bongo fleva kama ilivyokuwa kwenye nyimbo zake
zilizotangulia.
“Nawashukuru mashabiki kwa kuniunga mkono kwenye kazi zangu, sina cha
kuwalipa zaidi ya kuwatayarishia kazi nzuri zaidi ambazo zitawaburudisha na
kuwapa mafunzo ndani yake,” alisema.
Steve alipata kutoa singo matata ikiwamo ya ‘One Love’ alioimba na
Baby Boy na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia
ya muziki huo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269