Banda la NSSF linavyoonekana kwa nje.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya maofisa waandamizi wa NSSF katika Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Ofisa Uendeshaji wa Masuala ya Kompyuta, Kassim Mwandoro akitoa ufafanuazi kuhusu huuma wanazotoa kwa watu waliotembelea banda la NSSF.
Mapokezi
Mtoto, Suleiman Mohamed Salum (15), ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Ufundi Mtwara akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Amina Mbaga.
Watu mbalimbali wakipata huduma.
Maelekezo.
Ofisa wa Wakala wa Bima wa NSSF, Issac Peter akitoa maelezo ya huduma wanazotoa.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (kulia) akiwa na Ofisa Uhusiano Mwandamizi (NSSF), Theopista Muheta.
Mwanachama wa Orwinda Saccos, Rosemery Mulamula akionesha mali mpya walizoleta katika Monesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa. Saccos hiyo imeweza kushiriki maonesho hayo baada ya kupata mkopo kutoka NSSF.
Ofisa Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Salvatory Hinju (kulia), akifafanua jambo kwa mteja George Robert
aliyetembelea banda la shirika hilo lililoko katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara
ya Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Meneja Kiongozi Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume, akitoa maelezo kwa Leonard Chacha Kitoka (kushoto) kuhusu miradi mbalimbali ya ujenzi inayofanywa na NSSF wakati mteja huyo alipotembelea banda la shirika hilo kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba. Katikati ni Mhandisi wa NSSF, John Ndazi.
Ofisa Matekelezo Sekta Binafsi wa NSSF, Ally Mkulemba akimuonesha mmiliki wa Nkoromo Blog, Bashir Nkoromo jinsi ya kujaza fomu za kujiunga na Uanachama wa Hiari wa NSSF.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269