Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dares salaam inayoandaa matamasha ya Pasaka na Krismwass Bw. Alex Msama anaendelea
vizuri baada ya kupata ajali mkoani Dodoma kisha kupelekwa katika
hospitali ya mkoa wa Dodoma na baadaye kuhamishiwa katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili katika wodi Kibasila namba 16 hivi sasa anaendelea
vizuri na amesema hali yake imekuwa ikiimarika tofauti na ilivyokuwa
Mwanzo, Aliiambia Fullshangwe jana hospitalini hapo kwamba mungu ni
mwema na ametenda miujiza yake ndiyo maana amekuwa akiimarika
kiafya.Mfanyakazi
wa Kampuni ya Dira Ally Makuburi akimjulia hali Mkurugenzi wa kampuni
hiyo Bw. Alex Msama ambaye amelazwa katika hospitali ya taifa ya
Muhimbili, kulia ni Musa Mkama mwandishi wa gazeti hilo pia. Mfanyakazi wa Kampuni ya Dira Musa Mkama
akimjulia hali Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Alex Msama ambaye
amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya kupata ajali
mkoani Dodoma. Mkurugenzi
wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akiwa na wafanyakazi wake
na baadhi ya ndugu na jamaa wakati walipokwenda kumjulia hali katika
hospitali ya taifa ya Muhimbili jana.
Your Ad Spot
Apr 15, 2014
Home
Unlabelled
ALEX MSAMA AENDELEA VIZURI MUHIMBILI
ALEX MSAMA AENDELEA VIZURI MUHIMBILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269