Breaking News

Your Ad Spot

Jul 4, 2014

MKOA WA DODOMA WASHEREHEKEA KUANZA KWA UJENZI WA MRADI WA BARABARA YA DODOMA (MAYAMAYA) - BABATI (BONGA)

 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchmbi (wa nne kutoka kushoto) akiwaongoza wadau waliofika kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi wa barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami kuomba Dua ili mradi huo ukamilike kwa wakati bila kukwamishwa na changamoto mbalimbali. Sherehe hizo zilifanyika mapema Julai Mosi, 2014 kijijini Kolo Wilayani Kondoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (wa pili kushoto) na ujumbe alioambatana nao wakikagua magari yanayotumika kwenye ujenzi wa barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami Mapema jana wakati wa maadhimisho ya kusherehekea kuanza kwa ujenzi wa mradi huo yaliyofanyika Kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa, wengine pichani ni wakandarasi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group inayojenga barabara hiyo kipande cha Bonga-Mela (88.8KM).
  Mkuu wa  Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akimkabidhi Dereva Abuu Ally Funguo ya kuwashia mitambo ya kujengea barabara kuashiria kuanza rasmi kwa Ujenzi wa Barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami wakati wa kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo zilizofanyika mapema Julai Mosi, 2014 kijijini Kolo Wilayani Kondoa, Kulia anayeshuhudia ni Mbunge wa Kondoa Kaskazini Mhe. Zabein Mhita.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (Katikati mwenye kilemba) na ujumbe alioambatana nao wakipatiwa maelezo ya mradi wa barabara kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kutoka kwa wakandarasi wa Kampuni inayojenga barabara hiyo ya China Railway Seventh Group wakati alipotembelea kambi ya kampuni hiyo  iliyopo kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa mapema Julai Mosi, 2014
 Wakandarasi wa Kampuni ya China Railway Seventh Group inayojenga barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kipande cha Bonga-Mela (88.8KM) kwa kiwango cha lami wakisikiliza salamu ya Mkuu wa Mkoa Dodoma (Hayupo pichani) wakati wa kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo zilizofanyika Julai Mosi, 2014 kwenye Kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, wadau, Mafundi na Wataalamu wa Kampuni ya China Railway Seventh Group inayojenga barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami kipande cha Bonga-Mela (88.8KM) wakiwa kwenye picha ya pamoja muda mfupi baada ya kumalizika kwa sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi huo wa barabara zilizofanyika Kijijini Kolo Wilayani Kondoa Mapema Julai Mosi, 2014.
Sehemu ya Wananchi wa Kijiji cha Kolo Wilayani Kondoa waliojitokeza kwa wingi kuadhimisha sherehe za kuanza kwa ujenzi wa mradi wa barabara ya kutoka Mayamaya Dodoma hadi Bonga Babati kwa kiwango cha lami wakisikiliza salamu za Mkuu wa Mkoa Dodoma (Hayupo pichani), Sherehe hizo zilifanyika mapema Julai Mosi, 2014. Picha na John Banda wa Pamoja Blog
 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages