Breaking News

Your Ad Spot

Nov 21, 2014

KINANA, NAPE WATINGA RUAGWA MKOANI LINDI, MAMIA WAJITOKEZA KUWALAKI



 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye uwanja wa Ruangwa Likangara tayari kuhutubia wakazi wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
 Wananchi wa Ruangwa wakionyesha furaha yao wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM kwenye uwanja wa mkutano Ruangwa Likangara.
 Wananchi wa Ruangwa wakiwa na mabango yaliyobeba ujumbe wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kujenga na kukiimarisha chama,Katibu Mkuu wa CCM ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye .
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Ruangwa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Ruangwa ambapo aliwaambia CCM inaimarika kutokana na kuwa na sera zenye kuleta maendeleo kwa Watanzania pamoja na kuthamini amani iliyopo nchini.

Umati wa wakazi wa wilaya ya Ruangwa wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wao wa CCM Taifa.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa wilaya ya Ruangwa waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza,Kinana amekuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa CCM kuzunguka nchi nzima ,kushiriki kwenye miradi mbali mbali ya maendeleo,kukagua ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 pamoja na kutoa elimu kwa wananchi hasa ya kujiunga na mfuko wa afya ya jamii.
 Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Majaliwa Kassim Majaliwa akihutubia wakazi wa Ruangwa ambapo alielezea katika kipindi chake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge ameshiriki shughuli mbali mbali za maendeleo jimboni kwake.
 Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Majaliwa Kassim Majaliwa akihutubia wananchi wa Ruangwa ambapo alichukua muda wa kutosha kufafanua kwa wananchi namna alivyotekeleza wakatoi wa kipindi chake kama Mbunge wa Jimbo wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye anafanya ziara katika mikoa ya Lindi na Mtwara
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Ruangwa ambapo alisema uongozi mbovu kwenye vyama vya ushirika ni chanzo cha kusababisha matatizo kwenye zao la korosho,aliwaambia wananchi hao hakuna sababu ya msingi ya kuwa na utitiri wa vyama vya ushirika.
 Wananchi wa kijiji cha Mibure wakiwa na furaha wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  kwenye kijiji chao kilichopo wilaya ya Ruangwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Mibure ambapo aliwapongeza uamuzi wao wa kujenga Zahanati ya kijiji kwa kushirikiana na Mbunge wao pamoja na Halmashauri.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Mibure ambapo aliwashauri vijana kujiunga vikundi na kufanya shughuli za ujenzi kwani kuna miradi mingi ambayo vijana wanaweza kupatiwa fursa ya kuifanya kwa gharama nafuu.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua jengo la zahanati ya kijiji cha Mibure ambacho kinajengwa na mafundi wa kawaida wa kijijini hapo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wananchi wa kata ya Chienjele wilayani Ruangwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kata ya Chienjele wilaya ya Ruangwa ambapo aliwaambia vijana kuwa bado kuna fursa nzuri nchini katika kuleta maendeleo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCMkata ya Nandagala wilayani Ruangwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia chanzo cha maji kwenye mto Ole kijiji cha Ng'au kata ya Mnachu wilaya ya Ruangwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda miti kwa ajili ya kutunza mazingira pamoja na vyanzo vya maji.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Ng'au Ole wilaya ya Ruangwa ambapo aliwahimiza kutunza mazingira kwa kutokata miti badala yake wapande miti kutunza vyanzo vya maji.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Nandagala ,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha chama mkoa wa Lindi.PICHA ZOTE NA ADAM MZEE

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages