* NI LA MT.MERU CURIOS& CRAFTS MARKET
SOKO la bidhaa za utamaduni
lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS& CRAFTS MARKET limetea kwa
moto usiku wa kuamkia leo na kuunguza bidhaa zote za wafanya biashara
zililopo katika soko hilo
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika
kufuatia soko la wafanyabiashara wa Vinyago na bidhaa mbalimbali za
kitalii la Maasai Market kuteketea kwa moto.
Mulongo ambaye alifatana na kamati ya Ulinzi na Usalama alishangaa kuona
maduka hayo ambayo yapo jirani na Kikosi cha Zima Moto kushindwa kuzima
moto na kusababisha hasara kwa wananchi.
"Sitakubali kuona uzembe unaendelea katika mkoa wetu,lazima watu
wawajibishwe kwa uzembe hasa Kikosi cha kuzima moto ambao mko karibu na
Ofisi za Chama Cha mapinduzi wilaya yalipo maduka haya"amesema Mulongo
Chanzo cha moto bado hakijaweza kufahamika huku maduka hayo yapatayo
188, huku yakiwa hayajaunganishwa na Umeme kwa lengo la kuepusha hatari
ya moto kwani bidhaa nyingi ni vinyago vinavyotengenezwa kwa mbao.
Habari picha kwa hisani ya woindeshizza
blog
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269