Naibu waziri
wa maliasili na utalii MAHAMUOD MGIMWA ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi
kusini akiwa katika moja ya ziara zake za wizara ya maliasili na utalii
Naibu waziri
wa maliasili na utalii MAHAMUOD MGIMWA ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi
kusini akiwa katika moja ya ziara zake za wizara ya maliasili na utalii na wengine ni viongozi wa TANAPANaibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMUOD MGIMWA ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini akiwa ziarani
Naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMUOD MGIMWA ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini akiwa na mkuu wa wilaya ya mufindi
na fredy mgunda ,iringa
Naibu waziri
wa maliasili na utalii MAHAMUOD MGIMWA ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi
kusini amewataka vijana kujituma na kutumia fursa mbalimbali ambazo zinatolewa
na serikali.
Akizungumza
na mtandao huu Naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMUOD MGIMWA alisema kuwa
vijana wengi wamekuwa wakibweteka kwa kutojituma kufanya kazi na kuendelea
kuilaumu serikali.
“Eti asubuhi
unawakuta vijana wamekaa kwenye vijiwe wakizungumza siasa na kucheza mabao
wakati hawajui mchana watakula wapi na jioni watarudi na nini nyumbani”alisema MAHMOUD
MGIMWA
MGIMWA
ameendelea kuwaomba vijana wengi wenye fursa ya kurudi au kuingia shuleni upya
warudi kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi wengi kutokana na mabadiliko ya
kiuchumi na sayansi na teknolojia na ndio sababu inayopelekea hata watu wazima
kurudi shuleni.
“Vijana
mnatakiwakujifunza kutoka kwa watu wazima ambavyo wamekuwa wakijituma kufanya
kazi kwa bidii na kujituma ilimradi kuwatengenezea watoto maisha mazuri pamoja
na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla”alisema MAHMUOD MGIMWA
Lakini Naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMOUD MGIMWA
ambaye ni mbunge wa jimbo la mufindi kusini
amewataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali
katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
MGIMWA ameeleza
kuwa wanawake waondoe hofu ya kugombea hasa kukiwa na ushindani wa wagombea
wanaume kwa kuogopa kuchafuliwa kwa mambo yasiyokuwepo.
Ameendelea
kusema kuwa wananchi wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na badala yake
wachague viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka katika chama chochote.
Aidha
ameongeza kuwa viongozi wawe na sera za kutekelezeka ili kuwatendea haki wapiga
kura wao hali itakayowafanya waaminike katika jamii.
Mbali na
hayo MGIMWA amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa
katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na
badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa kiongozi kutokana
na sera za chama chake.
Ameendelea
kusema kuwa vijana wajitokeze kwa wingi katika kupiga kura ndiyo katika katiba
iliyopendekezwa ili kuweza kufanya uchaguzi ulio wa haki na amani pia
kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura pamoja na kupiga
kura.
Amemaliza
kwa kuwataka wananchi wa jimbo la mufindi kusini kuwa na imani nae kwa kuwa
amefanya yote ambayo aliwaahidi katika uchaguzi wa mwaka wa 2010 na amewaomba
waendelee kuwa na imani naye katika kutekeleza mambo mapya ambayo wamejitokeza
kwa lengo la kuleta maendeleo ya jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269